Mwombaji ambaye ni mara yake ya kwanza atatakiwa aambatishe barua ya utambulisho toka kwa kiongozi wake, cheti cha usajili wa taasisi na picha mbili aina ya passport size.
Kama ni maombi ya kuhuisha leseni, ambatisha leseni yako ambayo muda wake umeisha pamoja na picha yako moja ya passport size.
Lipa ada ya maombi ya Tsh 30,000/=
Tanbihi: Mkuu wa Taasisi ya Dini husika anapaswa kujaza form ya RGMF 2 (Endapo utajiombea mwenyewe, itakulazimu maombi yako yapitie kwa Mkuu wa Wilaya yako, ambaye atatoa maoni kuhusu ombi lako).
Ambatisha nakala ya Kiingereza au Kiswahili ya cheti chako cha ndoa (iwapo cheti chako cha ndoa hakiko katika Kiingereza au Kiswahili cheti kilichotafsiriwa na ofisa anayehusika au mthibitishaji wa umma.
Ambatisha kopi ya pasi ya kusafiria ya wanandoa.
Ambatisha nakala mbili za pasport size
Lipa ada inayotakiwa, kwa sasa ni Tsh. 100,000/=.
TANBIHI: Ndoa iliyofungwa katika balozi za Tanzania za ng’ambo zinachukuliwa kama ndoa zilizofungwa Tanzania bara ambazo hazikufuata utaratibu huu.