Swahili   |   English
Maulizo Mfululizo

NDOANA TALAKA (MAULIZO MFULULIZO)

  1. Ninawezaje kupata nakala ya cheti cha ndoa iwapo cheti halisi kilipotea?
    • Ndoa zote zinazofanyika Tanzania bara husajiliwa na kupata usajili wa msajili mkuu wa ndoa na talaka.  Wasajili wote wa wilaya na viongozi wa dini wanatakiwa kisheria kutuma ndoa zote walizozifungisha kila mwishoni mwa mwezi.  Kupitia katika taarifa hizi msajili mkuu kutunza kumbukumbu zote za ndoa.
    • Iwapo cheti halisi kimepotea unaweza kupata nakala ya usajili ya ingizo la ndoa ambalo  huhifadhiwa na msajili mkuu.

      Jinsi ya Kufanya ;
    • Wasilisha maombi yako kwenye ofisi za RITA ukionyesha majina ya wanandoa, mahali ilipofungwa, wilaya pia  onyesha iwapo ni ndoa ya kiserikali au ya kidini.
    • Lipa ada halisi ambayo kwa sasa ni Tsh. 30000/= inayojumuisha yafuatayo:
      - TSH 10000/= ada ya utafutaji.
      - TSH 20000/= ada ya cheti.


  2. Mimi ni Mtanzania ninayeishi ng’ambo na ninataka kuoa/kuolewa kulekule lakini mamlaka zinanitaka kuwapatia cheti kutoka Tanzania ambacho hakuna kipingamizi cha ndoa. Ninawezaje kukipata?
    • Nenda kwenye ubalozi wa Tanzania katika nchi unayoishi kupata fomu halisi ya maombi (kwa RGM...) ambayo utapaswa kuijaza na kuiwasilisha kwa msajili mkuu wa ndoa kupitia katika ubalozi au (unaweza kupakua fomu hii kutoka kwenye tovuti yetu) au iwasilishe katika ofisi za RITA nchini Tanzania ikitokea upo hapa.
    • Maombi haya lazima yaambatane na nyaraka muhimu zinazoweza kukutambulisha kirahisi.  Nyaraka hizo zinajumuisha japo si lazima nakala ya pasipoti, cheti cha kuzaliwa na sheria yoyote ya ndoa.
    • Lipa ada muhimu ambayo kwa sasa ni Tsh. 200,000/=.

      Tanbihi:
      Iwapo cheti hiki kitapaswa kutumwa kwako hakikisha kuwa malipo yanajumuisha gharama zozote za posta.


  3. Mimi ni Mtanzania ninayeishi ng’ambo. Nilifunga ndoa kule. Ninaweza kuisajili ndoa hii Tanzania?
    Ndiyo:
        Unaweza kuisajili ndoa hii kwa kuomba kwa msajili mkuu (ofisi za RITA).
      • Jaza fomu ya RGMF 7 na 48.
      • Ambatisha nakala ya Kiingereza au Kiswahili ya cheti chako cha ndoa (iwapo cheti chako cha ndoa hakiko katika Kiingereza au Kiswahili cheti kilichotafsiriwa na ofisa anayehusika au mthibitishaji wa umma.
      • Lipa ada inayotakiwa, kwa sasa ni Tsh. 29,000/=.

        TANBIHI:
        Ndoa iliyofungwa katika balozi za Tanzania za ng’ambo zinachukuliwa kama ndoa zilizofungwa Tanzania bara ambazo hazikufuata utaratibu huu.
    ^JUU  


  4. Kuna ndoa inayopaswa kusajiliwa na ninaona kuwa kuna vipingamizi kwenye ndoa hiyo, ninaweza kuviepuka?
    • Toa taarifa za vikwazo vyako kwa kuandika kwa msajili ambaye alipewa taarifa za mambo hayo.
    • Andika taarifa za vikwazo vyako kwa msajili mkuu wa ndoa na talaka
    • Iwapo unafikiri kuwa wana ndoa wanaweza kuamua kutoa taarifa mpya kwa msajili mwingine, andika vikwazo hivyo kwa msajili huyo.


  5. Ndoa nyingi zilivunjwa na mahakama.  Ninawezaje kupata cheti cha talaka yangu?
    • Wasilisha nakala ya cheti chako cha ndoa kwa msajili mkuu (RITA).
    • Wasilisha nakala ya uvunjaji ya mahakama
    • Lipa ada ya lazima ambayo kwa sasa ni Tsh. 20000/=

      TANBIHI:
      Talaka yako itatambuliwa na kusajiliwa  iwapo muda uliowekwa kwa rufaa utakuwa umekwisha na hakukuwa na rufaa iliyokubaliwa na iwapo ilikubaliwa ilikwishasikilizwa na hakuna rufaa zaidi.


  6. Inawezekana kwa mtu kuchukua kibali cha ndoa kwa niaba ya mtu mwingine?
    Ndiyo:
    • Kinachotakiwa ni kuleta kitambulisho chako, nakala halisi ya kibali kilichokwisha na barua ya utambulisho kutoka kwa mwombaji.


  7. Kwa ndoa iliyofungwa mwaka 1958 kabla ya sheria ya ndoa ya 1971 haijaanza na ndoa yangu haikusajiliwa kwa sheria ya zamani (Sheria ya ndoa) lakini ndoa yangu bado inadumu.  Ninaweza kuisajili ndoa hii na kupata cheti cha ndoa?
    Ndiyo:
    • Omba kwa msajili mkuu wa ndoa (RITA) kwa kujaza fomu za RGMF . 7 na 48.
    • Ambatisha ushahidi kwenye maombi haya kuthibitisha ndoa yako mfano cheti kilichotolewa na kiongozi wa dini au kadhi.
    • Ambatisha hati ya kiapo kuthibitisha kuwa ndoa hiyo bado inadumu.
    • Lipa ada muhimu ambayo kwa sasa ni Tsh. 20000/

VIZAZI NA VIFO (MAULIZO MFULULIZO)

  1. Mimi ni Mtanzania niliyezaliwa ng’ambo; ninaweza kupata cheti cha kuzaliwa kutoka ofisini kwako?
    • Mtanzania aliyezaliwa ng’ambo hawezi kupata cheti cha kuzaliwa Tanzania bara. Sheria inayoongoza usajili wa vizazi na vifo hairuhusu kusajili matukio ya vizazi vilivyotokea ng’ambo.

  2. Cheti changu cha kuzaliwa kina majina niliyopewa baada ya kuzaliwa, na nyaraka zangu nyingine zina majina tofauti, ninawezaje kulishughulikia tatizo hili?
    • Sheria inaruhusu kubadili majina ndani ya miaka miwili baada ya usajili wa kizazi. Njia mbadala ya ubadilishaji jina inaweza kufanywa kwa usajili wa jina la hati Sura ya 117

  3. Nilizaliwa nyumbani miaka mingi iliyopita; ninaweza kupata cheti changu cha kuzaliwa?
    • Ndiyo. Cheti cha kuzaliwa kinaweza kupatikana kwa maombi ya usajili uliochelewa kwa kujaza Fomu ya B3. 
      Tanbihi: Suala hili lisiwe lilitokea kabla ya Aprili, 1921.

  4. Baba yangu alikufa miaka mingi iliyopita, ninahitaji cheti chake cha kifo, nitakipataje?
    • Taratibu za kupata cheti cha kifo ni kusajili tukio la kifo kwanza kwa kujaza Fomu ya maombi ya D3 

  5. Ni taratibu zipi za kupata nakala ya cheti cha kuzaliwa baada ya kupotea?
      Toa maelezo sahihi yafuatayo:
    • Jina la mtoto
    • Jina la baba.
    • Jina la mama.
    • Mahali pa kuzaliwa.
    • Tarehe sahihi ya kuzaliwa na usajili.
    • Tarehe kilipotolewa iwapo kuna uwezekano.
    • Nakala ya cheti hicho kama ipo.
    • Ada halisi ya Tsh. 3500/=

  6. Mwenye jukumu la kusajili kifo ni nani?
    • Mwenye jukumu la kusajili kifo ni kama ifuatavyo:- Daktari, ndugu wa karibu wa marehemu aliyekuwepo wakati wa kifo.
    • Mtu aliyemhudumia wakati wake wa mwisho wa ugonjwa.
    • Mwenye nyumba.
    • Mpangaji.
    • Mtu yeyote aliyechukua jukumu la maziko ya marehemu.

  7. Mtoto wangu alizaliwa MWANZA; ninaweza kupata cheti chake cha kuzaliwa Dar es Salaam?
    • Unaweza kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto aliyezaliwa Mwanza iwapo tu Uzazi huo kwanza ulisajiliwa Mwanza. 
      Tanbihi: Vinginevyo, cheti cha kuzaliwa lazima kipatikane Mwanza.

  8. Makosa yanayoweza kufanywa wakati wa uandaaji cheti yanaweza kurekebishwa?
    • Marekebisho ya makosa hufanywa pindi mtu anapoomba.
    • Mwombaji lazima awasilishe nyaraka za thibitisha yaani nakala za vitambulisho au vyeti inayotakiwa ni Sh. 6500/= kwa uthibitisho.
    • Ada inayotakiwa ni Sh. 6500/=