Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Mfumo wa Usajili wa Uzazi

Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (PO – PSM) wanatekeleza mfumo wa Usajili wa Uzazi uliyoboreshwa (BRS) ambao ni kipengele muhimu katika mkakati wa RITA kusajili watoto wengi nchini Tanzania katika miaka mitano ijayo. Kuna umuhimu wa haraka wa kuboresha mfumo wa usajili wa uzazi. Idadi ya watoto waliozaliwa bila kusajiliwa inaongezeka kwa haraka sana na hujumuisha idadi kubwa ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. BRS ni mradi maalumu utakaoanzisha mfumo mpya kabisa wa kusajili uzazi kwa kutumia teknolojia mpya ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

BRS itaweza kuhakikisha kuwa watoto wote wachanga wanaozailiwa husajiliwa katika kipindi cha siku 90 baada ya kuzaliwa, ni lazima pia iwezeshe, wakati wote wa maisha yao, usajili wa idadi kubwa ya watu ambao kuzaliwa kwao hakukusajiliwa . Vifaa vya ukusanyaji taarifa na takwimu vya kisasa zaidi na mfumo ya mawasiliano vitatumika kujenga mfumo wa BRS wenye ubunifu na ufanisi. Katikati yake kutakuwa na kituo cha data salama kinachoingizwa taarifa mpya kila mara, ambacho kitatoa na kuhifadhi data kwa ajili ya mchakato wa usajili na kutegemea mahitaji/masharti ya usalama na uaminifu kutimizwa, kwa mashirika mengine ya Serikali.

Manufaa yanayotarajiwa.

  • Tija na ufanisi wa mfumo wa usajili muhimu kuwa bora zaidi;
  • Uwezo wa kufanyiza ripoti na data kuhusu hali ya wananchi/raia kuwa bora zaidi.
  • Mazingira mengi na bora kwa ajili ya kuhifadhi data na fursa za kuunganishwa na wanufaike wengine kama vile Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mfumo wa Utoaji Pasipoti, TRAUTUMISHINIDA, Kazi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)Mambo ya NdaniAfyaElimu n.k.
  • Ulinzi bora zaidi wa data za nchi nzima kuhusu takwimu muhimu, takwimu za usajili wa uzazi ni muhimu zaidi kwa utayarishaji mipango wa uhakika kuhakikisha kuwa mahitaji ya watoto ya msingi yanatimizwa.