Swahili   |   English
Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17

 

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umebuni mkakati ya Usajili na Kutoa vyeti katika Shule za Msingi katika Mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania Bara.

Zoezi hili  ni sehemu ya utekelezazji wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17 ( 5-17 Birth Registration Initiative) uliobuniwa ili kukabiliana na changamoto ya wananchi wengi kutosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

RITA imeshirikiana na idara ya Elimu kuendesha mkakati huu katika kila Mkoa na Wilaya Husika. Tangia mkakati huu kusimikwa umeshatekelezwa katika Wilaya zifuatazo: Musoma,Tarime,Bariadi,Singida,Songea,Bunda, Maswa,Kahama,Njombe, Tunduru, Kinondoni, Ilala na zingine ziko katika mpango wa kufikiwa na mkakati hii.

Programu hili ya Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 5-17 ni endelevu kwa Wilaya zingine na Mikoa yote Tanzania Bara.