Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           BRS4G MKOA WA DAR ES SALAAM

Description: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na viongozi wengine wa Mkoa kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kujisajili ili wapate vyeti vya Kuzaliwa. Mhe. Makonda aliyasema hayo katika Semina iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa viongozi hao kuwashirikisha maboresho yanayoendelea kufanyika Katika Mfumo wa Usajili kupitia Mkakati wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu (Civil Registration and Vital Statistics – CRVS) na Maboresho ya Mfumo wa Tehama katika Usajili (Birth Registration Syestem 4th Generation – BRS4G), Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar es Salaam.

Album Pictures