Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           RITA YAKABIDHIWA MALI YA ITOA

Description: RITA YAKABIDHIWA MALI ZA TAASISI YA ITOA YA NJOMBE Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka ameamuru mali za Umoja wa Wakulima wa Chai Igominyi (Igominyi Tea Outgrowers Association - ITOA) ya Mkoani Njombe kukabidhiwa kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa ajili ya kuzisimamia baada ya kubainika Taasisi hiyo haina Bodi ya Wadhamni iliyo hai na katika kipindi cha Mpito cha kuibadili Taasisi Hiyo kuwa Ushirika. Mheshimiwa Sendeka alitoa maamuzi hayo katika kikao alichoitisha kikishirikisha Viongozi wa Mkoa na Wilaya, RITA na Viongozi wa ITOA ili kupokea Ripoti ya Timu ya Wataalamu iliyoundwa na RITA kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko.

Album Pictures