Description:
Watoto wapatao 584,658 kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bure kwa kipindi cha miezi mitatu ya awali ya utekelezaji wa mpango maalum wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ulioanza kutekelezwa katika Mikoa ya kilimanjaro na Tanga.
Akihutubia wananchi hii leo katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Wizara yake inaendelea kusimamia kwa karibu pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kufanikisha kutekeleza mpango huo katika Mikoa yote Tanzania Bara.