Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           USAJILI WATOTO RUKWA KATAVI

Description: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi hii leo katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi amezindua rasmi Mpango wa Usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wa Mikoa ya Rukwa na Katavi. Kupitia hotuba yake Mhe. Prof. Kabudi ametoa maagizo kwa viongozi wa Mikoa hiyo miwili na mingine inayopakana na nchi jirani kusimamia zoezi hilo kwa uadilifu na umakini kwa kushirikiana na taasisi nyingine za utambuzi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa ni wale wanaostahili tu ambao wamezaliwa na watakaozaliwa ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.

Album Pictures