Description:
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Pauline Philipo Gekul (Mb) leo Machi 17, 2023 amefanya ziara na kuzungumza na Menejimenti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA). Hii ni ziara yake ya kwanza RITA tangu kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mwezi Februari 2023.