Swahili   |   English
Bodi ya Ushauri ya Wizara (MAB)

BODI YA USHAURI YA WIZARA (MAB)

 

Majukumu ya Bodi ya ushauri ya Wizara (MAB)


Bodi ya Ushauri ya Wizara ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili  ya kumshauri Waziri kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wakala.


Bodi ya Ushauri ya Wizara itatoa ushauri kwa Waziri  juu ya mambo  yafuatayo:

  • Maendeleo na urekebishaji wa muundo wa sera.
  • Malengo ya RITA.
  • Ukubalifu wa mkakati na mpango wa shughuli na bajeti zinazohusika za Kabidhi Wasii Mkuu.
  • Uwekaji wa vipaumbele na malengo ya utendaji kwa mwaka wa Wakala.
  • Ukubalifu wa ripoti za Mwaka na Taarifa za fedha.
  • Tathmini ya Utendaji wa Baraza.
  • Na suala lingine lolote lililomo kwenye Sheria ya Wakala Na. 30 ya 1997.
  • Masuala mengine yoyote zaidi yanayohusu RITA pale Afisa Mtendaji Mkuu atakapoona umuhimu kwa nyakati mbalimbali yataelekezwa kwenye Bodi.