RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
USAJILI
`
Kifo
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

1. MAOMBI YA CHETI CHA KIFO                                                        

Kifo husajiliwa na Kibali cha mazishi hutolewa katika kituo cha tiba tukio lilipotokea au kwa kifo kinachohusiana na polisi ni mpaka uthibitisho kutoka kwa Madaktari. Kifo kinachotokea nyumbani kinaweza kusajiliwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata. Tafadhali kumbuka, usajili wa kifo lazima ufanyike ndani ya siku 30, baada ya hapo kifo kitasajiliwa chini ya usajili uliochelewa.

MAHITAJI YA JUMLA KWA MAOMBI YA CHETI CHA KIFO

1)    kibali cha mazishi kutoka kituo cha tiba

2)    Muhutasari wa kikao cha wanandugu wa marehemu kumteua msimamizi wa mirathi na barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kata/kijiji ambapo tukio la kifo limetokea.

3)    Kadi ya kupigia kura au kitambulisho cha utaifa wa marehemu.

4)    Kitambulisho cha msimamizi wa mirathi na kinaweza kuwa kimoja wapo kati ha hivi; kadi ya mpiga kura, pasi ya kusafiria au kitambulisho cha utaifa.

5)    Cheti cha ndoa au vyeti vya watoto vya kuzaliwa.

TARATIBU ZA USAJILI WA KIFO

Hii inaweza kufanywa kwa kuzingatia yafuatayo:

1.     mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kuchagua huduma inayohitajika.

2.     Mwombaji atatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa kwake ili kuthibitisha akaunti.

3.     Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.

4.     ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza maombi ya usajili wa kifo nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa zako kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako.

5.     Mwombaji awe na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuviambatanisha baaada ya kukamilisha zoezi la kujaza taarifa katika mfumo nyaraka hizo ni kama zifuatavyo;

·Â  kibali cha mazishi kutoka kituo cha tiba

·Â  barua ya uthibitisho wa kifo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata

·Â  Muhutasari wa kikao cha wanandugu wa marehemu kumteua msimamizi wa mirathi na barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kata/kijiji ambapo tukio la kifo limetokea.

·Â  Kadi ya kupigia kura au kitambulisho cha utaifa wa marehemu

·Â  Kitambulisho cha msimamizi wa mirathi na kinaweza kuwa kimoja wapo kati ha hivi; kadi ya mpiga kura, pasi ya kusafiria au kitambulisho cha utaifa.

·Â  Cheti cha ndoa au vyeti vya watoto vya kuzaliwa (kama mwombaji ni mke/mume au mtoto).

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

(i)    Ada ya utoaji wa cheti kupitia mfumo kwa matukio ya vifo yaliyosajiliwa ndani ya muda Tshs 7000

(ii)   Ada ya usajili wa kifo kilichochelwa kuandikishwa ni Tsh 8,000 kwa tukio lililo chini ya miaka 10 na Tsh 20,000 kwa tukio zaidi ya miaka 10.

(iii) Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa.  

Endapo utakuta:

·Â Â Â Â Â Â  Neno “verify” ina maana maombi yamepelekwa hatua ingine kwa ajili ya kuhakikiwa na Msajili

·Â Â Â Â Â Â  Neno “return to client” ina maana maombi yana kasoro na yamerudisha kwa mteja kwa ajili ya kufanyia kazi malekezo ya Msajili halafu urejeshwe maombi hayo kwa ajili ya kuchakatwa.

·Â Â Â Â Â Â  Neno “approved” ina maana maombi yamekidhi vigezo na yamepelekwa kwenye hatua ya kuchapishwa cheti.

(iv) Neno “issued” ina maana cheti chako tayari. Ingia katika akaunti yako bonyeza neno submitted ikishafunguka utabonyeza details utaona neno download ibonyeze utaona fomu yako ya maombi ichapishe na ipeleke ofisi uliochagua kuchukua cheti chako.  

(v)   Angalizo, Tunapenda kusisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu na pia tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti kwa ajili yakutumia mfumo na kuingia kuangalia maombi yako kama yamepitishwa.

(vi) MUHIMU: Kama umesahau nywila (Password) unaweza kufanya marekebisho kwa kuponyeza neno “reset” inayopatikana pembeni ya neno “forget password” halafu kisha rudi katika email yako uliyoitumia kufungulia akaunti utakuta ujumbe wa kureset Password bonyeza ili kuhuisha akaunti yako ambapo utathibitisha (Confirm) baada ya hapo utatengeneza nywila mpya kwaajili ya kuingia (log in) katika mfumo na kutuma maombi.

2. UHAKIKI WA VYETI VYA VIFO

Ili uweze kuhakiki cheti cha kuzaliwa au kifo ingia kwenye mfumo kwa kutumia “link” ya huduma za RITA  https://erita.rita.go.tz/auth au unaweza kutumia tovuti ya Wakala www.rita.go.tz na kisha utabofya katika menu ya eRITA.

Namna ya kutuma maombi aya uhakiki wa vyeti

·Â Â Â Â Â Â  bonyeza huduma ya verification

·Â Â Â Â Â Â  jaza taarifa zinazohitajika

·Â Â Â Â Â Â  ambatanisha nakala laini ya cheti chako cha kuzaliwa au cha kifo kwa ajili ya uhakiki

·Â Â Â Â Â Â  Mfumo utatengeneza ankara “bill” ya shilingi 6,000/= kwaajili ya kuitumia kufanya malipo

·Â Â Â Â Â Â  Mwombaji atafuatilia maombi yake kwa kuingia (log in) katika akaunti yake.

·Â Â Â Â Â Â  Mwombaji atapokea majibu kwenye akaunti yake. Ilia aone majibu atatakiwa kubonyeza neno “submitted” ikisha funguka utabonyeza details utaona hali ya ombi

 

3. HUDUMA YA KUBADILISHA CHETI CHA ZAMANI KUWA KIPYA

Vyeti vya zamani ambavyo vilitolewa kabla ya vyeti vya kieletroniki vinabadilishwa kupitia huduma hii ili kuwawezesha wananchi kupata vyeti vipya vinavyotolewa kieletroniki.

JINSI HUDUMA INAVYOFANYIKA

1)    Mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kisha kuchagua huduma inayohitajika.

2)    Mwombaji atatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mwombaji ili kuthibitisha akaunti.

3)    Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.

4)    Mwombaji ataingia katika mfumo wa eRITA na kisha kubonyeza maombi ya kizazi baada ya hapo mwombaji atabonyeza kitufe cha “Old to New”. Baada ya hapo mwombaji atajaza taarifa zake kwa usahihi na kuchagua sehemu atakayo chukua cheti chake

5)    Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) ya cheti chake cha kuzaliwa kinachotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuambatanisha pamoja na viambata viwili kati ya vifuatavyo:

a.     kibali cha mazishi kutoka kituo cha tiba

b.     Muhutasari wa kikao cha wanandugu wa marehemu kumteua msimamizi wa mirathi na barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kata/kijiji ambapo tukio la kifo limetokea.

c.     Kadi ya kupigia kura au kitambulisho cha utaifa wa marehemu.

d.     Kitambulisho cha msimamizi wa mirathi na kinaweza kuwa kimoja wapo kati ha hivi; kadi ya mpiga kura, pasi ya kusafiria au kitambulisho cha utaifa.

e.     Cheti cha ndoa au vyeti vya watoto vya kuzaliwa.

6)    Mfumo utatengeneza Control Number ya malipo ya shilingi 8,000/= kwa ajili ya kufanyia malipo.

4. MAOMBI YA KUFANYA MAREKEBISHO KATIKA VYETI VYA VIFO

Huduma hii kwa sasa haipo kieletroniki na hivyo kuhitaji mwombaji kufika katika Ofisi zetu za Makao Makuu au Wilaya.

Marekebisho ya Jina la Marehemu

Marekebisho katika ya Sheria Usajili wa Vizazi na Vifo Sura ya 108 yaliyofanyika mwaka 2019, na kuruhusu marekebisho ya majina ya marehemu kama kuna herufi zimekosewa na sio kubadilisha jina lote au kuondoa majina ya marehemu.

Maombi hayo yatawasilishwa kwa barua kwa Msajili Mkuu na kuambatisha nyaraka za uthibitisho pamoja na kulipia ada iliyowekwa, na endapo maombi yatakidhi vigezo marekebisho hayo yatafanyika katika daftrari la usajili.

Angalizo; Jina linafanyiwa marekebisho na sio kufuta au kuondoa majina ya awali ya marehemu.

MAHITAJI YA JUMLA

·Â Â Â Â Â Â  Barua ya kuomba marekebisho

·Â Â Â Â Â Â  Cheti halisi kinachotakiwa kurekebishwa

·Â Â Â Â Â Â  Viambata vinavyothibitisha marekebisho yanayohitajika mfano kadi ya kura au NIDA, vyeti vya shule, pasi ya kusafiria N.K

·Â Â Â Â Â Â  Affidavit inaweza kuhitajika

·Â Â Â Â Â Â  Ada ya malipo ya shilingi 13,000/=

UTAMBUZI WA CHETI CHA KIFO KILICHOTOKEA NJE YA NCHI

Usajili wa Kifo hufanyika katika nchi ambayo kifo hicho kimetokea bila kujali asili ya marehemu. Nchi husika ambapo tukio la kifo limetokea inawajibika na kulazimika kimataifa kutoa nyaraka ya kutambua tukio hilo

Msajili Mkuu atakitambua kifo kilichotokea nje ya Tanzania iwapo tu mahitaji yafuatayo yatatimizwa;

       i.          Cheti cha kifo kilichopatikana kutoka kwa mamlaka ya kigeni ambayo ina mamlaka ya kutoa cheti cha kifo au ripoti ya kitabibu ikithibitisha kifo kutoka hospitali ambapo marehemu amefariki.

      ii.          Pasipoti ya marehemu;

    iii.          Hati ya kuzaliwa ya marehemu, ikiwa ipo;

    iv.          barua ya kuthibitisha kifo kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini ambako kifo kilitokea;

     v.          Cheti cha Kifo kilichoandikwa kwa lugha ambayo sio ya Kiswahili wala kingereza lazima kitafsiriwe na baraza la Kiswahili Tanzania.

    vi.          Ada ya shilingi 30,000/=

KIFO CHA ZAMANI KILICHOTOKEA ZAIDI YA MIAKA KUMI (10)

Familia zinahimizwa kusajili kifo mapema kinapotokea na kupata cheti cha kuthibitisha kifo hicho kwa sasabu uthibisho wa kifo ambacho kimetokea ndani ya muda mfupi ni rahisi kuliko uthibitisho wa kifo ambacho kimetokea muda mrefu kwani upatikanani wa nyaraka za kuthibirisha kifo hicho huwa ni mgumu.

Aidha endapo familia zitashindwa kusajili kifo kwa wakati na muda wa zaidi ya miaka kumi ukapita tokea kifo kitokee mwombaji atakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatavyo ili aweze kupata kusajili kifo na kupata cheti: -

  1. Muhutasari Kamati ya ulinzi na usalama ya kata, ikiongozwa na mtendaji wa kata pamoja na mtendaji wa kijiji/mtaa marehemu alipokuwa akiishi. Wajumbe wote wa kikao hicho watatakiwa waambatishe vitambulisho vya Nida au Kura na pamoja na picha zao. Kwenye muhutasari lazima mambo yafuatayo yawekwe bayana kuhusu taarifa za marehemu nayo ni:

a)    Marehemu alifariki lini na kuzikwa lini?

b)    Alizikwa makaburi gani?

c)     Marehemu alicha mke/wake, watoto na wajukuu wangapi?

d)    Marehemu aliacha mali gani na ziko wapi?

e)    Taarifa yoyote ambayo hatuifahamu kuhusu marehemu ambayo

inayoweza kutusaidia katika uchakataji wa maombi.   

  1. Aidha kwenye muhutasari huo kutakuwa na majina na saini ya kila mtu atakayehojiwa kwa ajili ya kuthibitisha kifo pamoja.
  2. Hati ya kiapo cha kuonyesha sababu za kuchelewa kusajili cheti cha kifo.
  3. Muhutasari wa kikao cha wanandugu wa marehemu kumteua msimamizi wa mirathi (mtendaji wa kata athibitishe muhutasari huo kuwa ni kikao halali kimefanyika ndani ya kata yake, asaini na kuugonga muhuri.). Muhutasari uambatishe majina ya wajumbe waliohudhuria na sahihi zao.
  4. Kitambulisho cha marehemu kinaweza kuwa kadi ya kupigia kura au kitambulisho cha utaifa. Pamoja na Kitambulisho cha mwombaji chenye picha inayoonekana.
  5. Barua ya kumtambulisha muombaji cheti cha kifo kutoka kwa Mtendaji kata (tukio la kifo lilipotokea na ieleze marehemu amefia sehemu gani mfano nyumbani/hospitali kata gani, mtaa, na aseme tarehe/mwezi/mwaka wa tukio la kifo lilipo tokea).

 

 

Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu