RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
USAJILI
`
Kizazi
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

RITA ni chombo cha serikali kilichokasimiwa jukumu la msingi la kusajilli Matukio Muhimu ya Binadamu ikiwemo vizazi na vifo. 

Jukumu hilo linasimamiwa na Sheria ya Usajili wa vizazi na Vifo Sura 108 ambayo imeweka ulazima wa kusajili kizazi na kifo kwa matukio yote yanayotokea Tanzania Bara. 

UMUHIMU WA USAJILI WA VIZAZI

(i)          Kuwa na haki ya kijamii: Matokeo ya uandikishaji ni kupata cheti cha kuzaliwa ambacho kinamruhusu kupata haki mablimbali za kijamii kama kujiunga na taasisi za elimu na baadae ajira za serikali, jeshi na taasisi za umma pamoja na binafsi.

(ii)            Kuwezesha kupata hati za kusafiria, kwani uhamiaji wataangalia taarifa zilizotolewa za wazazi, pamoja na kuhakikisha tarehe na mahali alikozaliwa muhusika.

(iii)         Kuweza kuthibitisha umri wa mtoto au mtu kwa madhumuni ya utekelezaji wa sheria mbalimbali kama sheria ya ajira, sheria ya ndoa, sheria ya uchaguzi, sheria ya kanuni ya adhabu n.k.

(iv)        Mtoto kupata haki ya utaifa ili kumwezesha kupata haki ambazo taifa linawajibika kutoa kwa raia wake.Kwa mfano, kwa sheria ya uraia ya Tanzania, endapo mzazi mmoja wa mtoto ni Mtanzania, basi mtoto huyo atakua ni raia wa Tanzania mpaka atakapofikisha umri wa miaka 18 ili aweze kuamua kama ataendelea kuwa raia wa Tanzania au vinginevyo.

(v)           Kuwezesha nchi (serikali) kuweka makisio sahihi katika mipango ya kijamii na maendeleo kulingana na idadi ya watu (takwimu). Mipango hiyo ni kama vile afya, elimu, maji, uchumi, ajira, mipango ya makazi n.k.

(vi)         Kuiwezesha serikali kujua ‘fertility rate’ ya mahali

(vii)        Kuwawezesha ndugu wa marehemu kupata stahili za marehemu ikiwa ni pamoja na; kufungua shauri la mirathi, kufuatilia miamala ya benki, kiinua mgongo na Bima mbalimbali.

(viii)       Kuwawezesha watoto wa marehemu kupata huduma za kijamii ; mfano mikopo ya elimu ya juu au misaada mbalimbali kutoka Serikalini na kwa jamii endapo itabainika watoto ni yatima.

UMUHIMU WA USAJILI KWA MIFUMO MINGINE

·Â Â Â Â Â Â  Mfumo wa vitambulisho vya Taifa (NIDA); Endapo mtu atafikisha miaka 18 atalazimika kutambuliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kama ni raia au mgeni au mkimbizi

·Â Â Â Â Â Â  Mfumo wa Daftari la wapiga Kura: Ili mtu aweze kuandikishwa kuwa mpiga kura lazima athibitishe kuwa ana umri wa utu uzima kulingana na sheria za Tanzania. Ni cheti cha kuzaliwa kitakachotoa uthibitisho huu.

·Â Â Â Â Mfumo wa utoaji Hati za Kusafiria: Ili upate Hati ya Kusafiria unatakiwa kuthibitisha miongoni mwa mambo mengine ulipozaliwa na wazazi wako ni akina nani.

·Â Â Â Â Â Â  Mfumo wa Sensa ya Watu na makazi: Iwapo mfumo wa usajili utaimarika itakuwa rahisi kujuwa idadi ya watu bila kulazimika kufanya zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo huwa ni aghali na hufanyika kila baada ya miaka kumi.

Usajili wa Matukio ya Vizazi na Vifo unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 108. Huduma zetu hizi kwa sasa zinapatikana kupitia mtandao (eRITA).

eRITA ni nini? eRITA ni mfumo unaokuwezesha kutuma maombi ya huduma ya VIZAZI kwa njia ya kidijitali popote ulipo. eRITA ni rahisi kutumia salama na itakuwezesha kupata huduma kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.

Ili kupata huduma zetu za mtandao, mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kuchagua huduma inayohitajika.

Maombi ya Cheti cha Kuzaliwa

Usajili wa kuzaliwa unaweza kufanywa katika:

i.              Katika kituo cha tiba au ngazi ya kitongoji kwa watoto wachanga (ndani ya siku 90)

ii.               Katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya (usajili wa kuchelewa)

iii.           Kwa mtandao (usajili wa kuchelewa, kubadilisha cheti cha zamani kuwa kipya)

Mtoto anasajiliwa mara tu baada ya kuzaliwa katika kituo cha tiba ambapo tukio la kizazi limetokea au katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata kwa vizazi vya nyumbani. Ikiwa kwa sababu fulani mtu anakosa kusajili mahali hapo, mtoto anaweza kusajiliwa wakati wa chanjo ndani ya siku 90. Aidha, tukio la kuzaliwa linaweza kusajiliwa kama usajili wa kuchelewa katika Ofisi ya Katibu wa Wilaya kwa kupitia mtandao.

Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa:

Mwombaji lazima aambatishe baadhi ya hati mbili kati ya zifuatazo:

  • Kadi ya Kliniki ya Mama
  • Kadi ya Kliniki ya Mtoto
  • Tangazo la kuzaliwa
  • Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
  • Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari - O Level)
  • Pasi ya kusafiria
  • Kadi ya mpiga kura
  • Cheti cha ubatizo

Pamoja na mojawapo ya haya:

  • Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
  • Hati ya kusafiria ya mzazi
  • Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata

N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai.

USAJILI UNAVYOFANYIKA KWA WATOTO WACHANGA
Mwombaji (Mzazi/mlezi) atasajili tukio hili kwenye dawati la Usajili katika Kituo cha tiba kizazi kilipotokea wakati mtoto anapozaliwa au wakati wa kupata chanjo. Pia Usajili unaweza kufanyika katika ofisi ya kata kwa vizazi vya nyumbani.

USAJILI KUPITIA ERITA (VIZAZI VILIVYOCHELEWA KUSAJILIWA)

1)    mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kuchagua huduma inayohitajika.

2)    Mwombaji anatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mombaji ili kuthibitisha akaunti.

3)    Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.

4)    ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza kizazi nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa zako kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako

5)    Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuviambatanisha pamoja na maombi yake katika mfumo nyaraka hizo ni kama zifuatavyo;

  • Kadi ya Kliniki ya Mama
  • Kadi ya Kliniki ya Mtoto
  • Tangazo la kuzaliwa
  • Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
  • Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari - O Level)
  • Pasi ya kusafiria
  • Kadi ya mpiga kura
  • Cheti cha ubatizo

Pamoja na mojawapo ya haya:

  • Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
  • Hati ya kusafiria ya mzazi
  • Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata

N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

(i)    Ada ya utoaji wa cheti kupitia mfumo kwa matukio ya vizazi yaliyosajiliwa ndani ya muda Tshs 7000

(ii)   Ada ya usajili wa kizazi kilichochelewa kuandikishwa ni Tsh 8,000 kwa tukio lililo chini ya miaka 10 na Tsh 20,000 kwa tukio zaidi ya miaka 10.

(iii) Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa.  

Endapo utakuta:

·Â Â Â Â Â Â  Neno “verify” ina maana maombi yamepelekwa hatua ingine kwa ajili ya kuhakikiwa na Msajili

·Â Â Â Â Â Â  Neno “return to client” ina maana maombi yana kasoro na yamerudisha kwa mteja kwa ajili ya kufanyia kazi malekezo ya Msajili halafu urejeshwe maombi hayo kwa ajili ya kuchakatwa.

·Â Â Â Â Â Â  Neno “approved” ina maana maombi yamekidhi vigezo na yamepelekwa kwenye hatua ya kuchapishwa cheti.

(iv) Neno “issued” ina maana cheti chako tayari. Ingia katika akaunti yako bonyeza neno submitted ikishafunguka utabonyeza details utaona neno download ibonyeze utaona fomu yako ya maombi ichapishe na ipeleke ofisi uliochagua kuchukua cheti chako.  

(v)   Angalizo, Tunapenda kusisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu na pia tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti kwa ajili yakutumia mfumo na kuingia kuangalia maombi yako kama yamepitishwa.

(vi) MUHIMU: Kama umesahau nywila (Password) unaweza kufanya marekebisho kwa kuponyeza neno “reset” inayopatikana pembeni ya neno “forget password” halafu kisha rudi katika email yako uliyoitumia kufungulia akaunti utakuta ujumbe wa kureset Password bonyeza ili kuhuisha akaunti yako ambapo utathibitisha (Confirm) baada ya hapo utatengeneza nywila mpya kwaajili ya kuingia (log in) katika mfumo na kutuma maombi.

2. UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA

Ili uweze kuhakiki cheti cha kuzaliwa au kifo ingia kwenye mfumo kwa kutumia “link” ya huduma za RITA  https://erita.rita.go.tz/auth au unaweza kutumia tovuti ya Wakala www.rita.go.tz na kisha utabofya katika menu ya eRITA.

Namna ya kutuma maombi aya uhakiki wa vyeti

·Â Â Â Â Â Â  bonyeza huduma ya verification

·Â Â Â Â Â Â  jaza taarifa zinazohitajika

·Â Â Â Â Â Â  ambatanisha nakala laini ya cheti chako cha kuzaliwa kwa ajili ya uhakiki

·Â Â Â Â Â Â  Mfumo utatengeneza ankara “bill” ya shilingi 6,000/= kwaajili ya kuitumia kufanya malipo

·Â Â Â Â Â Â  Mwombaji atafuatilia maombi yake kwa kuingia (log in) katika akaunti yake.

·Â Â Â Â Â Â  Mwombaji atapokea majibu kwenye akaunti yake. Ilia aone majibu atatakiwa kubonyeza neno “submitted” ikisha funguka utabonyeza details utaona hali ya

ombi.

3. HUDUMA YA KUBADILISHA CHETI CHA ZAMANI KUWA KIPYA

Vyeti vya zamani ambavyo vilitolewa kabla ya vyeti vya kieletroniki vinabadilishwa kupitia huduma hii ili kuwawezesha wananchi kupata vyeti vipya vinavyotolewa kieletroniki.

JINSI HUDUMA INAVYOFANYIKA

1)    Mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kisha kuchagua huduma inayohitajika.

2)    Mwombaji atatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mwombaji ili kuthibitisha akaunti.

3)    Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.

4)   Mwombaji ataingia katika mfumo wa eRITA na kisha kubonyeza maombi ya kizazi baada ya hapo mwombaji atabonyeza kitufe cha “Old to New”. Baada ya hapo mwombaji atajaza taarifa zake kwa usahihi na kuchagua sehemu atakayo chukua cheti chake.

5)    Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) ya cheti chake cha kuzaliwa kinachotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuambatanisha pamoja na viambata viwili kati ya vifuatavyo:

·Â Â Â Â Â Â  Kadi ya Kliniki ya Mama

·Â Â Â Â Â Â  Kadi ya Kliniki ya Mtoto

·Â Â Â Â Â Â  Tangazo la kuzaliwa

·Â Â Â Â Â Â  Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)

·Â Â Â Â Â Â  Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari - O Level)

·Â Â Â Â Â Â  Pasi ya kusafiria

·Â Â Â Â Â Â  Kitambulisho cha NIDA

·Â Â Â Â Â Â  Kitambulisho cha Mpiga kura

Pamoja na mojawapo ya haya:

·Â Â Â Â Â Â  Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi

·Â Â Â Â Â Â  Hati ya kusafiria ya mzazi

N.B: Hii itatumika ikiwa wazazi wapo hai

6)    Mfumo utatengeneza Control Number ya malipo ya shilingi 8,000/= kwa ajili ya kufanyia malipo.

4. MAOMBI YA KUFANYA MAREKEBISHO KATIKA VYETI VYA KUZALIWA

Huduma hii kwa sasa haipo kieletroniki na hivyo kuhitaji mwombaji kufika katika Ofisi zetu za Makao Makuu au Wilaya.

Marekekbisho ya Jina la Mtoto

Marekebisho katika ya Sheria Usajili wa Vizazi na Vifo Sura ya 108 yaliyofanyika mwaka 2019, na kuruhusu marekebisho ya majina ya mtoto pale ambapo kizazi kilisajiliwa kabla ya kupewa jina au kizazi kilisajiliwa na kupewa jina lakini jina hilo limebadilishwa, mzazi au mlezi anaweza, muda wowote kabla mtoto hajafikisha miaka 18 kupeleka maombi kwa Msajili ya kutaka jina libadilishwe.

Maombi hayo yatawasilishwa kwa barua kwa Msajili Mkuu na kuambatisha nyaraka za uthibitisho pamoja na kulipia ada iliyowekwa, na endapo maombi yatakidhi vigezo marekebisho hayo yatafanyika katika daftrari la usajili.

Angalizo; Jina linalobadilika ni la mtoto na sio majina ya wazazi.

Marekebisho ya herufi kwenye cheti cha kuzaliwa

Marekebisho ya herufi zilizokosewa kwenye cheti yanawezekana kufanyika kwa mwombaji kuwasilisha barua na viambatisho vinavyoonesha usahihi wa taarifa zake ili aweze kufanyiwa marekebisho kama yatakidhi vigezo. Endapo jina lililokosewa ni la mzazi mwombaji awasilishe kitambulisho cha mzazi husika, kama taarifa ni za mwombaji mwenyewe atawasilisha vitambuliisho vyake mfano cheti cha ubatizo, kadi la Klinik, vyeti vya shule N.K.

MAHITAJI YA JUMLA

·Â Â Â Â Â Â  Barua ya kuomba marekebisho

·Â Â Â Â Â Â  Cheti halisi kinachotakiwa kurekebishwa

·Â Â Â Â Viambata vinavyothibitisha marekebisho yanayohitajika kama jina lililokosewa ni la mzazi utakuja na kitambulisho cha mzazi husika kama taarifa ni zako utakuja na vitambuliisho vyako mfano cheti cha ubatizo, kadi la clinic, vyeti vya shule.

·Â Â Â Â Â Â  Affidavit inaweza kuhitajika

·Â Â Â Â Â Â  Ada ya malipo ya shilingi 13,000/=

UTAMBUZI WA CHETI CHA KUZALIWA KILICHOTOKEA NJE YA NCHI

Usajili wa Kizazi hufanyika katika nchi ambayo kizazi hicho kimetokea bila kujali asili ya mtoto. Nchi husika ambapo tukio la kizazi limetokea inawajibika na kulazimika kimataifa kutoa nyaraka ya kutambua tukio hilo. Ili ombi lako liweze kufanyiwa kazi inabidi uambatanishe viambatisho vifuatavyo;

1)    Cheti cha kuzaliwa kilichotolewa na mamlaka za usajili mahali ambapo mtoto amezaliwa au kadi la kliniki au taarifa za kitabibu kutoka hospitali aliyozaliwa mtoto

2)    Pasi ya kusafiria ya mtoto pamoja na vitambulisho vya wazazi.

3)    Cheti kilichoandikwa kwa lugha ngeni kitafsiriwe kwenda Kiswahili na Baraza la Kiswahili Tanzania.

4)    Ada ya shilingi 6,000/=

N: B Barua ya utambuzi itatolewa baada ya siku 3-5 za kazi.

 

Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu