RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
`
Muunganisho ya Wadhamini
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

JE MDHAMINI NI NANI?

Ni mtu au mwanachama wa chombo au bodi ya taasisi aliyepewa mamlaka ya kusimamia mali za chombo au bodi ya taasisi hiyo kwa mujibu wa sheria kulingana  na malengo/madhumuni yaliyokusudiwa.

LENGO LA KUSAJILI BODI ZA WADHAMINI

Muunganisho wa Wadhamini unaviwezesha vyombo vilivyounganishwa kuwa na sura ya kisheria kuweza kushitaki au kushitakiwa kwa jina lake, kumiliki na kuuza mali.

Aina za Bodi za Wadhamini

Taasisi za dini, Vyama vya         Siasa, Vyama vya kijamii, Vyama vya michezo n.k.

WAJIBU NA MAJUKUMU YA WADHAMINI

a)     Hawaruhusiwi kupata/kumiliki ardhi, fedha, hisa n.k bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa Wadhamini.

b)     Kuleta marejesho ya wadhamini kila baada ya miezi 12 kuisha/kumalizika baada ya usajili.

c)     Kumuarifu Kabidhi Wasii Mkuu mabadiliko yoyote ya wadhamini, jina la chama /taasisi, anuani au Katiba   (taarifa itolewe ndani ya mwezi mmoja baada ya tukio)

d)     Mdhamini lazima atende kulingana na mapatano/masharti ya katiba ya chama/taasisi na sheria husika.

e)     Mdhamini anapaswa kutenda kazi yake kwa kwa maslahi bora ya chama/taasisi.

f)      Mdhamini hatakiwi kuonekana anapata manufaa au faida yoyote binafsi.

g)     Mdhamini anapaswa kujua ukomo wa nafasi yake kwa mujibu wa Katiba ya chama/taasisi.

h)     Mdhamini azijue rasilimali zote na madeni yote ya chama/taasisi yake na afahamu utendaji au uzembe wa wadhamini wa zamani na hali /hadhi ya chama

i)       Pale ambapo mtu atakapoacha kuwa mdhamini na pale ambapo mdhamini mpya atateuliwa na ambapo mdhamini atabadilisha jina lake au makazi au anwani lazima Msimamizi Mkuu wa Wadhamini aarifiwe kwa maandishi na mdhamini ndani ya mwezi mmoja katika fomu maalumu.

MAMLAKA YA MSIMAMIZI MKUU WA WADHAMINI

n  Anaweza kuchunguza au kumuidhinisha mtu sahihi amchunguze mdhamini kwa niaba yake

n  Kutengua au kumuondoa mdhamini na mtu yeyote atakayethibitika kutumia au kufuja mali za taasisi/chama

n  Kumteua kamati ya mpito au mdhamini wa umma kutunza mali hiyo na kuendesha shughuli za kila siku za chombo wakati uteuzi wa mdhamini/mdhamini mpya unasubiriwa.

n  Kufunga Akaunti ya Benki ya Chombo/chama.

n  Kusimamisha matendo zaidi ya mdhamini/wadhamini katika kushughulika na mali ya chombo/chama.

n  Kurejesha tuhuma kwa Mamlaka za Uchunguzi zaidi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwa lengo la kuchukua hatua zaidi za kisheria Mahakamani.

n  Kufuatilia mdhamini/wadhamini ambao wamevunja mkataba/mapatano ya chombo/chama na kuokoa mali na kutafuta fidia.

UFUATILIAJI WA MIKUTANO YA VYOMBO, VYAMA/USHIRIKA

n  Lazima kuwe na mkutano halali wa chombo/ushirika au chama kwa madhumuni ya kuchagua mtu au watu kama wadhamini wa chombo au chama hicho.

n   Wadhamini lazima Kushiriki katika Kupitishwa kwa azimio lolote la kubadili katiba au sheria ya chama  kama ipo na kama mabadiliko hayo yanaathiri mamlaka au majukumu ya wadhamini au uteuzi wao au umiliki wa mali au amana ambayo wao ni wahusika

n  Kwa vyombo vya kidini ni lazima kufuatiliwa na mamlaka zao kuu husika hapa Tanzania kwa mujibu wa mkataba na amri za mamlaka hizo, au vyombo hivyo.

Miunganisho ya Wadhamini unaviwezesha vyombo visivyoshirikishwa kuwa na uwezo binafsi wa kisheria wa kufungulia na kufunguliwa shitaka katika jina la asasi, kumiliki mali na kuachia mali.

Taratibu / Mahitaji:

  • Wasilisha Fomu ya Maombi TI.1 na kiambatanishi "A" ikiambatishwa na Waraka wa Katiba ya asasi unaoomba kushirikishwa (Nakala 3).
  • Wasilisha picha ndogo 3 za wadhamini waliopendekezwa, na wasifa wao.
  • Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo chombo hicho kina makao yake makuu.
  • Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika sekta ya Serikali ambapo asasi inayotaka kuunganisha wadhamini wake inaangukia (kama ni asasi isiyo ya kidini).
  • Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika asasi kuu za kidini iwapo kinachoomba ni asasi ya kidini.
  • Lipa ada halisi/ada ya sasa ni Tsh. 200,000/=.

Tanbihi:

 1: Msimamizi Mkuu wa Wadhamini halazimika kuunganisha muunganisho wa Wadhamini pindi mahitaji ya hapo juu yasipotekelezwa.
  1. Nyaraka zote zinazowasilishwa ziwe Nakala mbilimbili isipokuwa Barua ya Mapendekezo.
  2. Mara baada ya kuunganishwa, muunganisho huu unakuwa na wajibu ufuatao:
    • Hairuhusiwi kumiliki ardhi au haki kwenye ardhi, bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa wadhamini (Kabidhi Wasii Mkuu).
    • Kumtaarifu Msimamizi Mkuu wa wadhamini juu ya mabadiliko yoyote, mabadiliko ya wadhamini, jina la chombo, anwani ya posta, Katiba ndani ya mwezi mmoja.
    • Kuwasilisha marejesho ya wadhamini kujaza fomu T.1.5 kila baada ya muda wa miezi kumi na miwili .
2: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo/au marekebisho yoyote kwa ujumla.
Taratibu / Mahitaji
  • Jaza na wasilisha Fomu ya TI.2 na TI.3.
  • Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu ya mkutano uliothibitishwa ambao ulifanya mabadiliko ya jina.
  • Rejesha cheti halisi cha zamani .
  • Lipa ada halisi Fomu za TI. 2 na TI. 3 Tsh 50,000/=
3: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya wadhamini.
Taratibu / Mahitaji
  • Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 4
  • Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi ambacho kilifanya mabadiliko ya Wadhamini.
  • Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
4: Marejesho ya Wadhamini.
Taratibu / Mahitaji
  • Jaza na wasilisha Fomu ya TI.5
  • Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
5: Taarifa ya kubadili anwani ya Posta.
Taratibu / Mahitaji
  • Jaza na wasilisha Fomu ya TI.6
  • Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
6:Taarifa ya kubadili Dhamana / katiba.
Taratibu / Mahitaji
  • Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 7
  • Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 50,000/=).
  • Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi kilichoamua mabadiliko ya dhamana / katiba.
7.Kupata kibali cha kumiliki ardhi.
Taratibu / Mahitaji
  • Wasilisha barua ya maombi ukielezea matumizi yanayokusudiwa ya ardhi .
  • Wasilisha nakala iliyodhibitishwa ya barua ya toleo/mkataba wa uuzaji/waraka wa ubadilishaji mmiliki.
  • Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
8.Upekuzi wa rekodi za Wadhamini.
Taratibu / Mahitaji
  • Wasilisha maombi ya upekuzi.
  • Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=
9.Kuthibitisha nakala ya Nyaraka.
Taratibu / Mahitaji
  • Wasilisha maombi
  • Lipa ada ya Tsh. 30,000/= ya uthibitisho wa nakala husika

10.Kupata nakala ya nyaraka

  • Wasilisha maombi
  • Lipa ada ya Tsh. 10,000/= kwa uthibitisho wa ofisi
Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu