WOSIA NI NINI?
n Wosia ni kauli/maandishi yanayotolewa au kuachwa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonesha nia yake ya namna angependa mali yake igawanywe baada ya kufa kwake.
n Wosia unaweza kuwa wa namna mbili;
nWosia wa mdomo
n Wosia wa maandishiÂ
Sifa za wosia wa maandishi:
Uandikwe kwa kalamu ya wino na sio kalamu ya risasi (inayoweza kufutwa)
n Muusia awe na akili timamu.
n Utaje tarehe ulipoandikwa.
n Utaje kuwa muusia anayo akili timamu na anausia kwa hiari yake mwenyewe na mali anayousia iwe yake.
n Ushuhudiwe na mashahidi wawili mmoja mwana ukoo na mwingine mtu baki kulingana na matakwa ya muusia.
n Usainiwe na muusia mbele ya mashahidi wake wakiona, au aweke alama ya dole gumba.
n Uwekwe saini za mashahidi ambao wamechaguliwa na muusia mwenyewe.
Sifa za Wosia wa Matamshi
n Ushuhudiwe na mashahidi wanne (wawili wa ukoo na wawili watu baki kulingana na matakwa ya muusia)
ANGALIZO
n Iwapo mashahidi watafariki kabla ya muusia muusia inabidi afanye marekebisho katika wosia wake.
n Mali ikiongezeka au kupungua mtoa wosia anaweza kufanya marekebisho hayo.
KUBATILISHWA WOSIA
Wosia waweza kubatilishwa ikiwa itathibitika kwamba
v Wakati akiandika au kutoa wosia, muusia alikuwa amepungukiwa akili kwa sababu ya wazimu, ugonjwa, ulevi au hasira ya ghafla.
ANGALIZO:
Warithi ndio wanaoruhusiwa kupinga wosia kwa sababu zilizoainishwa
Mrithi Kunyimwa Urithi na Muusia
v Kulingana na Sheria ya Usimamizi wa Mirathi,
muusia anaweza kumnyima mrithi urithi wake ikiwa mrithi;
i.                Amezini na mke wa mtoa urithi
ii.               Amejaribu kumuua, amemshambulia au amemdhuru vibaya mtoa urithi au mama mzazi wa mrithi
iii.             Bila sababu ya haki, hakumtunza mtoa wosia kutokana na njaa au hali ya ugonjwa
iv.             Ameharibu mali ya muusia, uharibifu wake utahesabika katika kukadiria kiwango cha urithi atakachostahili kupata
FAIDA ZA KUANDIKA NA KUTUNZA WOSIA NA RITA;
i.                Ni taasisi ya Serikali isiyo na ukomo wa maisha
ii.               Ina sehemu salama ya kutunza Wosia
iii.             Ina wanasheria wataalamu waliobobea katika masuala ya Mirathi
iv.             Gharama zake ni nafuu
v.               Ni Taasisi ya Serikali hivyo hujali maslahi ya wanufaika na kuyapa kipaumbele kwa mujibu wa Sheria.
KUBATILISHWA KWA WOSIA
¢ Wosia unaweza kubatilishwa ikiwa itathibitika kwamba;
i.      Wakati akiandika au kutoa wosia, muusia
alikuwa amepungukiwa akili kwa sababu ya wazimu, ugonjwa, ulevi au ghafla.
ii.     Muusia awe na akili timamu