Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi.
Utaratibu wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa, kwa Watu Walio nnje ya Nchi.
Hatua ya Kwanza:
Tuma barua pepe ya maombi kupitia info@rita.go.tz
Ambatanisha na kimojawapo kati ya viambatanishi vifuatavyo (Clinic card, Cheti cha ubatizo, School leaving certificates [Shule ya msingi, Sekondari]), kwa uhakika wa tarehe ya kuzaliwa mtoto, sehemu ya uzaliwa na uraia wa wazazi.
Pakuwa fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya siku 90, lakini chini ya miaka 10), au fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya miaka 10). Jaza na zitume kwa barua pepe info@rita.go.tz Fomu za kupakuwa zinapatikana hapa
Hatua ya Pili:
Utapokea barua pepe kutoka RITA, iliyoambatanishwa na fomu ya Afidavit, kutoka kwa Msajili Mkuu.
Printi na jaza fomu ya Afidavit, kisha iambatanishe na picha 3 za passport size.
Scan fomu ya Afidavit, itume kwa barua pepe kuelekea info@rita.go.tz
Hatua ya Tatu:
Utapokea barua pepe kutoka RITA, ikikupa ruhusa ya kulipia.
Malipo ya kusafirisha cheti yatategemea huduma utakayoamua kutumia (DHL, EMS n.k)
Malipo:
Cheti cha mtoto chini ya miaka 10 - $14.
Cheti cha mtoto zaidi ya miaka 10 - $20.
ku-clear cheque - $20.
Tanbihi:
Utatakiwa ufanye uchunguzi ili kufahamu Malipo ya kusafirisha Cheti ni bei gani, halafu utume fedha (ya kulipia cheti), pamoja na fedha ya kukombolea mzigo(fedha).