Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
HUDUMA ZA SIMU ZA RITA

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ,inahuduma mbalimbali za simu. RITA katika kuboresha zaidi huduma zetu, tumeweka mfumo wa kuwaweka wateja wetu karibu na sisi na sisi kua karibu na wateja wetu. Tunahuduma za simu ili wateja wetu wasilazimike kupata usumbufu wa kwenda mpaka ofisi za RITA kupata taarifa kuhusu huduma zetu.

Huduma zetu za simu zitaiwezesha umma kujua huduma za RITA kwa kupokea ujumbe mfupi wa maandishi. Wateja wa RITA wanaotaka kujua kwa ufupi namna ya kusajii matukio kama vizazi na vifo, wanaweza kutuma neno RITA kwenda 15584 na kupokea muongozo utakaomuwezesha kujua ni taratibu gani zinafuatwa kusajili matukio yaliyotokea katika mazingira mbalimbali kwa mfano usajili wa kizazi kilichotokea hospitali na kwengine.

Pia huduma nyingine nyingi ziko mbioni ili kuhakikisha wateja wetu wanapata taarifa na huduma zetu kwenye viganja vyao muda wowote na pahali popote. Huduma hii kila meseji itagharimu Tsh.200.