Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
UJUMBE WA KAIMU MTENDAJI MKUU

Wateja wetu wapendwa,

 

Karibuni katika Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambayo tunaamini itakuwezesha kupata Taarifa za Kina na sahihi za huduma na masuala mengine mengi kuhusu Wakala.

RITA ni Taasisi ya Serikali inayotoa huduma za aina 17 kwa wadau mbalimbali na kati ya hizo zipo ambazo ni za msingi zinazomlenga moja kwa moja kila mwananchi.

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya taarifa kuhusu Huduma zinazotolewa, RITA imeona iko haja ya kuongeza wigo wa njia za mawasiliano na Wadau kwa kuanzisha Tovuti hii ambayo itaenda sambamba na kuongezeka kwa matumizi ya Teknolojia katika mawasiliano ya umma.

Tovuti hii inatoa taarifa mbalimbali kuhusu majukumu/kazi za Wakala, Sheria ,Miongozo na Kanuni kuhusu huduma za Usajili, Ufilisi na Udhamini. Vilevile utaweza kupata taarifa kuhusu Mikakati na Programu mbalimbali zinazotekelezwa na Wakala ambazo lengo lake ni kuboresha upatikanaji wa huduma zetu kote nchini.

Tovuti hii inakupa fursa ya kupata maelezo ya kina kuhusu huduma zote hivyo kukuwezesha Mwananchi kujiandaa kikamilifu kabla ya kuja kuomba huduma katika Ofisi za Wakala.

Vilevile tovuti hii inakupatia nafasi ya kupakua fomu za maombi ya huduma, kuuliza maswali au kutuma maoni na malalamiko na kupata taarifa za matukio muhimu yanayotokea RITA.

Tunaahidi kuendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu huduma zetu na tutafurahi kupata maoni yako kuhusu Tovuti na huduma tunazozitoa kwani maoni yako yatasaidia sana katika kuboresha huduma zetu kwa wananchi.

 

ASANTENI  SANA.


Emmy K. Hudson,

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)


Pia unaweza kutufuatilia katika mitandao ya kijamii kama vile

Facebook: www.facebook.com/ritatanzania

Twitter: RITATanzania

YouTubewww.youtube.com/ritatanzania

RITA Mobile: TUMA neno RITA kwenda 15584