RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
`
Ndoa na Talaka
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

NDOA NA TALAKA

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ina jukumu la kusimamia usajili wa ndoa, kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za ndoa Tanzania Bara. Aidha ina jukumu la kusajili, kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za talaka zinazotolewa na Mahakama. Usajili wa Ndoa na Talaka unaongozwa na Sheria ya Ndoa Sura ya 29 Toleo la 2019.

NDOA

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa Sura ya 29 Toleo la 2019 Ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanamke na mwanaume, unaokusudiwa kuwa wa kudumu  kwa muda wa maisha yao yote.  Kwa minajiri ya tafsiri hii hakuna ndoa ya muda, baina ya watu wa jinsi ya aina moja au Ndoa ya Mkataba.

AINA ZA NDOA

Kuna aina mbili za ndoa:

¨Â Â Â Â Â  Ndoa ya mke mmoja

¨Â Â Â Â Â  Ndoa ya wake wengi au inayokusudiwa kuwa ya wake wengi

 

WAFUNGISHA NDOA

Mamlaka ya kufungisha ndoa imewekwa kwa: wafuatao:

¨Â Â Â Â Â  Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya kwa ndoa za KISERIKALI.

¨Â Â Â Â Â  Viongozi wa Dini (Maaskofu, Mapadre, Wachungaji, Masheikhs n.k) wenye Leseni hai za kufungisha ndoa, ambazo hutolewa na Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka ambaye ni Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA).

¨Â Â Â Â Â  Kwa ndoa za KIMILA zifungwe mbele ya Afisa Mwandikishaji ambaye ni Afisa Tarafa husika wa sehemu ile ndoa inapofungwa na kuandikishwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

USAJILI WA NDOA

Ni wajibu wa Mfungisha Ndoa kuisajili ndoa aliyoifungisha na kutoa cheti cha ndoa mara tu baada ya ndoa hiyo kufungwa. Kwa kuzingatia hili ni vyema Mfungisha Ndoa kabla ya kufungisha ndoa kuhakikisha anazo Shahada za Ndoa zinazotolewa na Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka kwa ajili ya kusajili ndoa na kutoa cheti cha ndoa. Ifahamike kuwa Uthibitisho wa ndoa ni cheti cha ndoa na wala si picha za harusi.

Ndoa isajiliwe kwa kujaza shahada ya ndoa RGM. 8 yenye nakala mbili na baada ya kuijaza wafunga ndoa watie saini zao mbele ya mfungisha ndoa na mashahidi wao. Vile vile mashahidi na mfungishai ndoa waweke saini zao kama shuhuda kwa ndoa iliyofungwa. Baada ya hayo kukamilika, mfungisha ndoa awapatie wana ndoa Shahada ya ndoa kila mmoja. Aidha, nakala moja ya shahada ya ndoa itabaki na mfungisha ndoa na nakala ingine itawasilishwa kwa Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka kila mwisho wa mwezi, ili ndoa zilizofungwa kwa mwezi husika ziwezwe kuandikishwa kwenye Daftari la ndoa la Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka

 

FAIDA ZA KUSAJILI NDOA; -

¨Â Â Â Â Â  Kutoa utambulisho kwa wanandoa kuwa ni mke na mume.

¨Â Â Â Â Â  Cheti cha ndoa ndio uthibitisho wa ndoa kisheria.

¨Â Â Â Â Â  Cheti cha ndoa kinampa mwanandoa haki ya urithi endapo mwenzi wake atafariki.

¨Â Â Â Â Â  Cheti cha ndoa kinamwezesha mwanandoa kupata haki mbali mbali zitolewazo na mwajiri wa mwenzi wake.

¨Â Â Â Â Â  Cheti cha ndoa kinamwezesha mwanandoa kudai haki ya matunzo au machumo ya pamoja endapo ndoa itavunjika.

 

 

USAJILI WA NDOA KWA NJIA YA MTANDAO

Ili kupata huduma yetu mtandaoni mwombaji anatakiwa kujisajili kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na bofya menyu ya eRITA kuchagua neno lililoandikwa Sajili hapa katika huduma za ndoa na talaka ili kujisajili kwenye mfumo. Mwombaji anapaswa awe na barua pepe iliyo hai ili aweze kuingia kwenye tovuti ya RITA www.rita.go.tz na kujisajili kwanza kabla ya kuomba huduma anayoitaka.


Jinsi ya kufanya maombi ya huduma mbalimbali:-

1. Maombi ya shahada ya kutokuwepo pingamizi

Ni nyaraka inayotolewa na Msajili Mkuu wa ndoa kuthibitisha kuwa raia wa Tanzania hana rekodi ya ndoa na hivyo ana sifa za kuolewa nje ya nchi.

Mahitaji yanayohitajika ili kupata shahada ya Kutokuwepo pingamizi:

- Cheti cha kuzaliwa

- Pasi ya kusafiria ya mwombaji,

- Barua ya uthibitisho kutoka kwa mzazi/mlezi,

- Kitambulisho cha mzazi/mlezi

- Pasi ya kusafiria/kitambulisho cha mtarajiwa anayekusudiwa

Jinsi ya kufanya Maombi

Ø  Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na atabonyeza palipoandikwa Jisajili hapa ili kufungua akaunti kwa kujaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa “Save”

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila kwa kubonyeza palipoandikwa “Click here to set password” kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba, mfano wa nywila ni uPendo@24

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la NDOA kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa Shahada ya kutokuwepo pingamizi na kufanya maombi mtandaoni, mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo. Gharama ni Tsh 300,000/=

Ø Waombaji watajulishwa kupitia akaunti yao ikiwa maombi yao yamekubaliwa au kukataliwa, Wanaweza pia kufuatilia hali ya maombi yao kupitia mfumo wa mtandaoni.

2. MAOMBI YA LESENI YA KUFUNGISHA NDOA.

Leseni ya kufungisha ndoa ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu wa Ndo ana Talaka ikimpa kiongozi wa dini mamlaka ya kufungisha ndoa. Msajili Mkuu anaweza kufuta leseni ya kufungisha ndoa wakati wowote kwa chapisho la kwenye Gazeti la Serikali.

Mahitaji yanayohitajika ili kuomba leseni kwa muombaji mpya:

·Â Â Â Â Â Â  Mwakilishi wa Taasisi ya Dini husika lazima awe amesajiliwa katika mfumo wa RITA.

·Â     Awe na kiambatisho. Kiambata kinaweza kuwa kati ya kitambulisho cha Taifa/ kadi ya kupigia kura/ pasipoti ya kusafiria/ Leseni ya udereva ambacho kinapaswa kiwe kwenye PDF.

·Â Â Â Â Â Â  Picha passport size kwenye PNG

Mahitaji yanayohitajika ili kuomba leseni kwa mwenye leseni ya zamani ambayo haijaisha muda wa matumizi

·Â Â Â Â Â Â  Mwakilishi wa Taasisi ya Dini husika lazima awe amesajiliwa katika mfumo wa RITA.

·Â Â Â Â Â Â  Leseni ya zamani ambayo haijaisha muda wake iwe kwenye PDF.

·Â Â Â Â Â Â  Picha passport size kwenye PNG

Jinsi ya kufanya maombi

Ø  Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na kubonyeza palipoandikwa Jisajili hapa ili kufungua akaunti kwa kujaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa “Save”

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila kwa kubonyeza palipoandikwa “Click here to set password” kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba.

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la NDOA kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa Leseni ya kufungisha ndoa. Atafanya maombi kwa kujaza taarifa zinazotakiwa; kama ni muombaji mpya au leseni ya awali haikuwa ya mfumo na ilishaisha muda wake ataomba kama muombaji mpya bila kuweka namba ya leseni na kuambatisha nyaraka zilizoanishwa mtandaoni ambazo ni kadi ya kupigia kura/kitambulisho cha Taifa/ pasipoti ya kusafiria/ Leseni ya udereva na picha ndogo passport size. Kama leseni ya awali haikuwa ya mfumo na muda wake hauijaisha au alishapata ya mfumo na imeisha muda ataambatanisha leseni ya zamani na picha pasiport size kwenye profile yake.

Ø  Sharti la awali la kusajiliwa ni kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Dini kusajiliwa katika mfumo wa RITA.

Ø  Mfumo utatoa namba ya malipo kwa Mwombaji na Mwombaji atalipa ada ya maombi. Malipo ni Tsh 60,000/=

3. KIBALI MAALUM CHA MSAJILI MKUU

Ni ruhusa maalum inayotolewa kwa wanandoa watarajiwa ya kufunga ndoa yao bila ya kutangazwa siku ishirini na moja (21). Kibali maalum cha kufunga ndoa hutolewa na Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka kwa kuzingatia sababu mbali mbali za msingi zinazotolewa na wanandoa wenyewe au Taasisi zao za dini. Kibali hicho kinaitwa “Ruhusa Maalum ya Msajili Mkuu (Registrar General’s Special Licence)”.

Msajili Mkuu anaweza kutohitaji taarifa ya kutangaza nia ya kufunga ndoa kama matakwa ya Sheria ya Ndoa inavyotaka pale ambapo kuna sababu ya kutosha ya kutotangaza nia kwa kufanya maombi kwa kuambatisha nyaraka zinazohitajika.

Mahitaji yanayohitajika ili kuomba kibali cha Msajili Mkuu

·Â Â Â Â Â Â  Vitambulisho au hati za kusafiria za wanandoa watarajiwa (PDF)

·Â Â Â Â Â Â  Picha aina ya passpoti ya wanandoa watarajiwa(PNG)

·Â Â Â Â Â Â  Kibali cha kutokuwa na ndoa (kuonyesha hali ya ndoa) kwa raia wa Kigeni (PDF)

·Â Â Â Â Â Â  Nyaraka inayoonyesha uharaka wa wahusika inayotoka mamlaka nyingine (mwaliko wa kwenda nje ya nchi/ uhamisho) ambayo ndio sababu ya kuomba kibali cha Msajili Mkuu.

Jinsi ya kufanya maombi:-

Ø  Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza kwa ajili ya mfumo ili kuendelea na maombi. Ikumbukwe kuwa mteja huyu atakuwa ameshaweka nia ya kufunga ndoa kwanza kabla ya kuomba kibali cha Msajili Mkuu cha kufunga ndoa bila kutangaza siku 21. Atabonyeza dirisha la ndoa kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa kibali maalum cha msajili mkuu.

Ø  Atabonyeza palipoandikwa Maombi kwa kujaza taaarifa zake na za mwenzi wake mtarajiwa na kuchagua sehemu (wilaya/taasisi) anayotaka kufungia ndoa  kisha kuweka viambata alivyoelekezwa vitakavyokuwa kwenye PDF na maombi hayo yataelekezwa kule alikochagua ili yapitishwe na kisha mfungishaji ndoa mhusika itayatuma kwa Msajili Mkuu kwa ajili ya kuyafanyia kazi na kibali kutolewa.

Ø  Maombi yanaweza kukubaliwa au kukataliwa

Ø  Malipo yatafanywa baada ya maombi kukubaliwa na kulipiwa pesa ya Tsh 200,000/=

Ø  Kibali kitatolewa

4. MAOMBI YA KIBALI CHA KUFUNGA NDOA MAHALI MAALUM

Ndoa hufungwa sehemu zilizoruhusiwa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 29 na 30 cha Sheria ya Ndoa Sura ya 29. Kifungu cha 29 kimeainisha kuwa ndoa za kiserikali zitafungwa katika ofisi za Msajili wa Ndoa wa Wilaya.  Aidha kifungu cha 30 kimeainisha kuwa ndoa zitafungwa kwa mujibu wa desturi za dini mahali popote ambapo wafuasi wa dini husika hukusanyika kwa ajili ya ibada. Msajili Mkuu anaweza kutoa kibali cha kufunga ndoa mahali maalum tofauti na mahali palipozoeleka kutumika kama mahali pa ibada au mikusanyiko baada ya kupokea maombi ya wenzi wanaotegemea kuoana.

Jinsi ya kufanya maombi:-

Ø  Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA . Mfumo wa ndoa na talaka ukifunguka Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza kwa ajili ya mfumo ili kuendelea na maombi. Ikumbukwe kuwa mteja huyu atakuwa ameshaweka nia ya kufunga ndoa kwanza kabla ya kuomba kibali cha kufungia ndoa mahali maalum

Ø Atabonyeza dirisha la ndoa kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa kibali cha kufungia ndoa mahali maalum kujaza taarifa na kuchagua mahali maalum nje ya kule kulikozoeleka. Mwombaji lazima aeleze mahali alipokusudia kufungia ndoa yake na kutuma maombi mtandaoni na nyaraka za kuthibitisha maombi.

Ø  Mwombaji atalipia Tsh 200,000/=

Ø  Kibali kitatolewa.

5.  NIA YA NDOA (INTENTION TO MARRY)

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa mwanamke na mwanaume wanaotarajia kufunga ndoa wana wajibu wa kutangaza nia ya kufunga ndoa siku 21 kabla siku ya kufunga ndoa.

Mahitaji yanayohitajika ili kuomba nia ya kufunga ndoa

-        Picha aina ya passpoti ya wanandoa watarajiwa

-        Vitambulisho au hati za kusafiria za wanandoa watarajiwa

-        Kibali cha kutokuwa na ndoa (kuonyesha hali ya ndoa) kwa raia wa Kigeni

-        Barua ya utambulisho toka ofisi za mtaa

Jinsi ya kufanya Maombi: -

Ø  Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na kubonyeza palipoandikwa Jisajili hapa kama ni mwombaji wa ambae ni mara ya kwanza kuingilia kwenye mfumo ili kufungua akaunti kwa kujaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa Save

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila kwa kubonyeza palipoandikwa Click here to set password kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba.

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la NDOA kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa nia ya kufunga ndoa ili aweze kufanya maombi kwa kujaza taarifa zake na za mwenza wake na kisha kuambatisha nyaraka.

Ø  Mwombaji lazima achague mahali alipokusudia kufungia ndoa yake wakati wa kufanya maombi.

Ø  Mwombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa, Anaweza pia kufuatilia hali ya maombi kwenye mfumo.

Ø  Mfumo utatoa namba ya malipo kwa ajili ya kulipia gharama ya huduma kufunga ndoa katika ofisi ya mkuu wa wilaya na mwombaji atafanya malipo ya sh. 100,000.

6.  MAOMBI YA KIBALI CHA KUTOKUWA NA NDOA

Ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu kuthibitisha kuwa muombaji wa hati hiyo kuwa hana ndoa.

Mahitaji  yanayohitajika ili kupata kibali cha kutokuwa na ndoa:

- Cheti cha kuzaliwa.

- Pasi ya kusafiria ya mwombaji,

- Barua ya uthibitishaji kutoka kwa mzazi/mlezi,

- Kitambulisho cha mzazi/mlezi

Jinsi ya kufanya Maombi: -

Ø  Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuchagua huduma za ndoa na talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na kubonyeza palipoandikwa Jisajili hapa kama ni mwombaji wa ambae ni mara ya kwanza kuingilia kwenye mfumo ili kufungua akaunti kwa kujaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa Save

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila kwa kubonyeza palipoandikwa Click here to set password kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba.

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la NDOA kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa kibali cha kutokuwa na ndoa na atafanya maombi na kuambatisha nyaraka zake,

Ø  Mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo ambayo ni Tsh 200,000/=

Ø  Mwombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa, Anaweza pia kufuatilia hali ya maombi kupitia mfumo wa mtandaoni.

Ø  Kibali kitatolewa.

7. USAJILI WA NDOA ZILIZOFUNGWA NJE YA NCHI

Msajili Mkuu ana mamlaka ya kusajili ndoa zilizofungwa nje ya nchi.

 Mahitaji  yanayohitajika ili kusajili ndoa iliyofungwa nje ya nchi

-        Cheti cha ndoa kilichothibitishwa na ubalozi wa nchi husika

-        Pass ya kusafiria za wanandoa

-        Picha pasipoti size za wanandoa

-        Cheti kitakachoambatishwa kama hakikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza kinapaswa kiambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza na afisa ubalozi wa nchi kinapotoka au na BAKITA kwa Tanzania.

 

Jinsi ya kufanya Maombi: -

Ø  Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz na kuchagua huduma za ndoa na talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na kubonyeza palipoandikwa Jisajili hapa kama ni mwombaji wa ambae ni mara ya kwanza kuingilia kwenye mfumo ili kufungua akaunti kwa kujaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa Save

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila kwa kubonyeza palipoandikwa Click here to set password kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba.

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la NDOA kisha zitatokea huduma za ndoa na atabonyeza palipoandikwa usajili wa ndoa zilizofungwa nje ya nchi ili afanye maombi maombi na kuambatisha nyaraka zilizoanishwa kwenye mfumo

Ø  Cheti kitakachoambatishwa kama hakikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili kinapaswa kiambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa nchi kinapotoka au na BAKITA kwa Tanzania.

Ø  Mwombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 200,000/=

 

8. USAJILI WA TALAKA

Talaka ni ruhusa au amri ya Mahakama ya kuvunja ndoa. Mahakama ndio chombo pekee chenye uwezo wa kuvunja ndoa. Aidha, matamko au maandishi ya kuvunja ndoa nje ya mahakama hizo si Talaka zinazotambuliwa na Sheria yetu ya Ndoa Sura ya 29.

Hatua za kufuata wakati wa kuomba Talaka

Mtu yeyote anayetaka kuomba Talaka Mahakamani lazima afuate taratibu zifuatazo;

¨Â Â Â Â Â  Kwanza, Mwenye nia ya kuomba ndoa yake ivunjwe anatakiwa kupeleka malalamiko ya matatizo yake ya ndoa kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la kamishina wa Ustawi wa Jamii au Baraza la la Ndoa lingine lolote linalotambuliwa kisheria kama vile Baraza la Kata, Kanisani au BAKWATA n.k

¨Â Â Â Â Â  Pili, Baraza la Usuluhishi la Ndoa litasikiliza malalamiko husika na kama litashindwa kuwasuluhisha wanandoa husika, litaandika hati maalum kwenda Mahakamani likielezea mgogoro huo kwa ufupi na kutoa maoni yake kuhusu suala walilosikiliza.

¨Â Â Â Â Â  Tatu Mlalamikaji atapeleka hati hiyo Mahakamni kwa ajili ya kufungua shauri lake la kuomba ndoa ivunjwe kisheria na haki zake nyinginezo kutamkwa na Mahakama.

 

Msajili Mkuu anatoa cheti cha talaka kwa maombi ya wahusika baada ya mahakama kutoa talaka. Huduma ya talaka hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa kwa kutoa cheti cha talaka.

Faida za kusajili talaka:-

¨Â Â Â Â Â  Kuwezesha kupata hati ya Talaka ambayo ni uthibitisho wa hali (status) ya ndoa ya mhusika.

¨Â Â Â Â Â  Kumwezesha mtalikiwa kupata haki ya kuoa au kuolewa tena na mtu mwingine

¨Â Â Â Â Â  Kuwezesha umma kujua kuwa ndoa imevunjika.

¨Â Â Â Â Â  Kulinda Mali ya mtalikiwa ili endapo atafariki mwenzi wake wa zamani kutaka kudai urithi.

¨Â Â Â Â Â  Kupata takwimu za ndoa zinazovunjika na wapi zinatokea

 

Mahitaji yanayohitajika ili kufanya maombi ya cheti cha talaka

-        Hukumu ya kuvunja ndoa/ kubatilisha

-        Hati ya talaka

-        Cheti cha ndoa

 

Jinsi ya kufanya maombi

Ø  Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka chini ya huduma ya ndoa na talaka abonyeze palipoandikwa Bofya hapa kupata huduma.

Ø  Mfumo wa ndoa na talaka utafunguka na kubonyeza palipoandikwa Jisajili hapa kama ni mwombaji wa ambae ni mara ya kwanza kuingilia kwenye mfumo ili kufungua akaunti atajaza taarifa zake kamili kama atakavyoelekezwa kwenye mfumo na akikamilisha kujisajili atabonyeza palipoandikwa Save

Ø  Mwombaji atapata ujumbe kwenye barua pepe yake aliyoiandika ili kutengeneza nywila(password) kwa kubonyeza palipoandikwa Click here to set password kwenye ujumbe aliopokea. Nywila inatakiwa iwe na herufi kubwa, herufi ndogo, alama maalum na namba.

Ø  Mwombaji ataweka barua pepe na nywila aliyotengeneza ili kuendelea na maombi. Atapata madirisha mawili ya NDOA na USIMAMIZI WA TALAKA. Atabonyeza dirisha la TALAKA maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo.

Ø  Muombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa,

Ø  Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 40,000/=

Ø  Cheti cha Talaka kitatolewa.

NB: Sharti la awali ni hukumu ya talaka lazima iwe imetolewa na mahakama yenye uwezo na mamlaka na kuwe hakuna rufaa au muda uliowekwa wa rufaa utakuwa umeisha

 

 

9. TALAKA ILIYOTOLEWA YA NCHI

Maamuzi ya mashauri ya ndoa yaliyotolewa na mahakama zenye mamlaka za nchi za nje yatatambulika na kusajili nchini Tanzania.

 

Mahitaji  yanayohitajika ili kufanya maombi

Ø  Hukumu ya kuvunja ndoa/ kubatilisha

Ø  Hati ya talaka ambapo haki ya kukata rufaa haipo tena na iwapo haikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au kiswahili inapaswa iambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa mamlaka husika.

Ø  cheti cha ndoa

 

Jinsi ya kufanya maombi

Ø  Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo

Ø  Mwombaji katika maombi yake lazima aainishe ni mahakama ya nchi gani iliyotoa hiyo talaka.

Ø  Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh. 200,000/=

Ø  Cheti cha Talaka kitatolewa.

 


 

 

 



Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu