Swahili   |   English
Usajili wa Talaka


TALAKA

RITA husajili Talaka na pia hutoa vyeti. Talaka husimamiwa na Sheria ya Ndoa 1971, Sura ya 29. toleo la 2002.

Mahitaji/Taratibu:
  • Wasilisha hati ya talaka ambapo haki ya kukata rufaa haipo tena (Iwapo ni hati ya kigeni inahitaji kwanza kutolewa chini ya sheria inayohusika). Hitaji hili litakuwa si lazima iwapo Mahakama iliyovunja ndoa itakuwa ilimtumia Msajili Mkuu nakala ya amri ya kuvunja ndoa kama inavyotakiwa na sheria.
  • Wasilisha Nakala ya Cheti cha Ndoa.
  • Ada halisi ya kupata nakala ya cheti cha Talaka 

BEI HUDUMA ZA USAJILI WA NDOA

 

NA

AINA YA HUDUMA 

ADA (Tzs)

1

Cheti cha Ndoa cha Msajili Mkuu wa Ndoa

 

40,000/=

2

Cheti cha Ndoa ambayo haijawahi kuandikishwa (Subsisting Marriage)

40,000/=

3

Cheti cha ndoa iliyofungwa nje ya nchi (Foreign Marriage)

200,000/=

4

Cheti cha Talaka

40,000/=

5

Cheti cha Talaka iliyotolewa nje ya nchi

200,000/=

6

Leseni ya kufunga ndoa mahali maalum

200,000/=

7

Shahada ya kutokuwepo pingamizi (Certificate of No Impediment)

300,000/=

8

Barua ya kutokuoa/kutokuolewa

200,000/=

9

Uthibitisho wa Cheti cha Ndoa au Talaka

40,000/=

10

Ada ya upekuzi katika daftari la Ndoa/Talaka

50,000/=

11

Kuandikisha uthibitisho wa ndoa iliyobadilishwa kuwa ya mke mmoja au ya wake wengi

40,000/=

12

Marekebisho katika cheti cha ndoa na talaka;-

Ada ya Upekuzi

Ada ya Marekebisho

Ada ya Cheti cha Msajili wa ndoa na talaka

 

40,000/=

 

50,000/=

13

Leseni ya Kufungisha Ndoa

60,000/=

14

Ndoa ya haraka

200,000/=

15

Ada ya ruhusa ya kufungisha Ndoa mahali maalum kwa mgonjwa

20,000/=

16

Ndoa ya Serikali ya kutangaza siku 21

100,000/=

17

 

 

Shahada ya ndoa zinazotolewa kwa

wasajili wa wilaya na viongozi wa

dini:-

Shahada 10

 

 

200,000/=

    

 

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU TALAKA