Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           KIKAO RITA NA BENKI YA DUNIA

Description: KIKAO CHA RITA NA BENKI YA DUNIA. Menejimenti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini [RITA] leo Februari 26,2024 jijini Dar es salaam imekutana na kufanya kikao na wawakilishi wa Benki ya Dunia na kuona namna RITA inavyofanya kazi. Akizungumza kwenye kikao hicho Naibu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Bi. Irene Lesulie amesema kuwa RITA imepiga hatua muhimu katika usajili wa matukio muhimu ya binadamu ambapo sasa matukio yote yanasajiliwa kwa njia ya kielektroniki kote nchini. Timu hiyo kutoka Benki ya Dunia imepata fursa ya kutembelea ofisi ya RITA muhimbili kuona namna usajili wa usajili wa vizazi na vifo unavyofanyika na kuipongeza kwa jitihada kubwa inazofanya.

Album Pictures