RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
July
20
2025
RITA AWAY DAY 2025
News & Update
`

Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi amewataka watumishi wa RITA kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa kutanguliza uadilifu na uaminifu ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Amezungumza hayo katika kikao cha kila mwaka cha Watumishi wa Wakala kutoka Mikoa yote kilichofanyika leo Julai 20, 2025 jijini Dar es salaam.

Bw. Kanyusi amesisitiza kuwa, watumishi wote wanatakiwa kuzingatia sheria na kaduni za utumishi wa umma ambazo kwa pamoja zimeweka bayana dhana nzima ya maadili na uwajibikaji katika kuleta ufanisi na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Aidha, kwa upande wao Watumishi wameupongeza uongozi na menejimenti ya  RITA kwa kuwakutanisha pamoja kujadilili pamoja changamoto na kuzitafutia majibu yatakayosaidia kuboresha utoaji wa huduma.

Wakati huo huo, watumishi wastaafu walikabidhiwa zawadi kama sehemu ya kuthamini mchango wao katika utumishi wa umma huku wakitumia siku hiyo kuagana na kutakiana kheri kwa watumishi wanaobaki kwenye utumishi huo.

Vile vile, baadhi ya Wilaya zimekabidhiwa zawadi kwa kufikia malengo na kuwa mfano bora katika utoaji wa huduma na elimu kwa wananchi, miongoni mwa wilaya hizo ni pamoja na Arusha.

Tags : #RITA