RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
Utangulizi
Karibu RITA

Kutoka kwa Kabidhi Wasii Mkuu

Napenda kuwakaribisha wananchi wote katika tovuti yetu ambayo imeboreshwa na kutengenezwa kwa umahiri mkubwa kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali kuhusu kazi na shughuli zinazotekelezwa  na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) hususani katika juhudi za kusaidia utoaji haki kwa wananchi kupitia huduma tunazotoa.

Tovuti hii ni nyenzo ya kukupatia taarifa sahihi na za kina kuhusu aina ya huduma tunazotoa, upatiakanaji wake na gharama husika kwa pamoja ikiambatana na Sheria 9 zinazoongoza majukumu ya wakala.  Aidha, tovuti hii ina video, picha na machapisho  mbalimbali kwa ajili ya umma na hivyo kuifanya kuwa ni miongoni mwa sehemu muhimu za marejeo kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wakala.

Wakala unaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma zake kwa njia ya kidijitali ambapo kwa sasa wananchi wanatumia mfumo wa eRITA kutuma maombi ya huduma za Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka pamoja na Udhamini. Tovuti hii ni dirisha muhimu linalomuwezesha mwananchi kuingia katika mfumo wa eRITA.

Natoa wito kwa wadau wote kuendelea kutembelea mara kwa mara Tovuti yetu na kuwasihi kuwasiliana nasi kwa maoni, ushauri na ufafanuzi zaidi juu ya huduma zetu kupitia njia mbalimbali zilizoainishwa.

Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora na kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati.

 

Bw. Frank K. Frank

Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu

Maono

Chanzo cha kuaminika katika utoaji wa taarifa za Usajili wa matukio muhimu ya binadamu,ufilisi na huduma za udhamini

Misheni

Kulinda haki za wote kwa kutoa huduma bora za usajili wa matukio muhimu,ufilisi na udhamini ili kufanya maamuzi sahihi .

Maadili ya msingi

Weledi, Uadilifu, Kumjali mteja, Uzalendo, Ubunifu na Ushirikiano

Frank Kanyusi Frank
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu
Maono

Chanzo cha kuaminika katika utoaji wa taarifa za Usajili wa matukio muhimu ya binadamu,ufilisi na huduma za udhamini

Misheni

Kulinda haki za wote kwa kutoa huduma bora za usajili wa matukio muhimu,ufilisi na udhamini ili kufanya maamuzi sahihi .

Maadili ya msingi

Weledi, Uadilifu, Kumjali mteja, Uzalendo, Ubunifu na Ushirikiano

Ona Zaidi
Pata Habari
Habari na Taarifa Mpya
RITA YAWASILISHA TAARIFA YA USAJILI NA USIMAMIZI WA BODI ZA WADHAMINI KWA KAMATI YA BUNGE UTAWALA, KATIBA NA SHERIA
Mar 25, 2025 News & Update

RITA) imewasilisha taarifa ya utekelezaji na usimamizi wa Bodi za Wadhamini wa Taasisi za Kidini, vyama vya Siasa, vyama vya Michezo na taasisi za kijamii kwa Kamati ya Bunge Utawala, katiba na Sheria.

MKUTANO WA WAJUMBE WA BODI ZA WADHAMINI
Mar 13, 2025 News & Update

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia wajumbe wa Bodi za wadhamini Jijini Dar es Salaam.

RITA KUANDAA SERA YA UWAJIBIKAJI KWA JAMII ILI KUYAFIKIA MAKUNDI YOTE YENYE UHITAJI
Sep 23, 2024 News & Update

Kabidhi Wasii Mkuu Bw. Frank Kanyusi leo Septemba 23, 2024 Jijini Dodoma amefungua kikao kazi cha kuandaa sera ya uwajibikaji kwa jamii.

Hakuna rekodi iliyopatikana

TANGAZO LA KUENDELEA KWA MNADA WA UUZAJI WA MALI CHAKAVU (MAGARI NA VIFAA MBALIMBALI VYA OFISI)
Apr 06, 2021 Procurement

ANNOUNCEMENT OF THE CONTINUATION OF THE DISPOSAL AUCTION OF VEHICLES AND VARIOUS OFFICE EQUIPMENTS

TANGAZO LA KUSITISHWA KWA MNADA WA UUZAJI WA MALI CHAKAVU (MAGARI NA VIFAA MBALIMBALI VYA OFISI
Mar 17, 2021 Procurement

ANNOUNCEMENT OF THE SUSPENSION OF THE DISPOSAL AUCTION OF VEHICLES AND VARIOUS OFFICE EQUIPMENTS

TANGAZO LA MNADA WA UUZAJI WA MALI CHAKAVU (MAGARI NA VIFAA MBALIMBALI VYA OFISI)
Mar 04, 2021 Procurement

AUCTION ANNOUNCEMENT OF VEHICLES AND VARIOUS OFFICE EQUIPMENT

TANAGZO KWA WAFUNGISHAJI NDOA
Jan 31, 2024 Announcement

TANAGZO KWA WAFUNGISHAJI NDOA

MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
May 04, 2023 Announcement

MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

Ona Zaidi
Tunachofanya
Huduma Zetu

Tovuti ya eRITA

eRITA ni jukwaa la mtandaoni lililoanzishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Tanzania kwa ajili ya usajili wa kielektroniki wa kuzaliwa, vifo, ndoa, talaka na usajili wa wadhamini.

Usajili

Usajili unawawezesha watumiaji kusajili matukio ya kuzaliwa, vifo, ndoa, na talaka mtandaoni. Unarahisisha uwasilishaji wa maombi, uhakiki wa nyaraka, na utoaji wa vyeti rasmi kwa ajili ya utambuzi wa kisheria na upatikanaji rahisi.

Ufilisi

Inasimamia usajili wa kufilisika na ufilisi wa kampuni, kuhakikisha utambuzi wa kisheria kwa watu binafsi au biashara zisizoweza kulipa madeni na kwa kampuni zinazovunjwa ili kutimiza majukumu ya kifedha.

Udhamini

Usajili na usimamizi wa mirathi, huduma za usimamizi mkuu wa umma, wadhamini waliosajiliwa, na wosia. Inahakikisha utambuzi wa kisheria, usimamizi sahihi wa mali, na uteuzi wa wadhamini kwa watu binafsi na taasisi.

You can check your application status

Simply dial our short code to instantly view the progress of your application, receive real-time updates, and stay informed on the go—quick, easy, and accessible anytime, anywhere.

*152*00*46#
Changua 3 RITA Services
  • *152*00*46#
  • Tuma neno ERITA ( weka namba ya ombi) kwenda 15200