RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
April
13
2026
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. DKT. JUMA HOMERA AZINDUA MKUTANO WA WAJUMBE WA BODI ZA WADHAMINI MKOANI RUVUMA
News & Update
`

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Homera amekemea ufujaji wa mali za taasisi, migogoro ya mara kwa mara na kung'ang'ania madaraka kwa muda mrefu unaofanywa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi za Wadhamini wa Taasisi za dini, Vyama vya michezo na Asasi za kiraia.

Waziri Dkt. Homera amesema hayo wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Bodi za Wadhamini kutoka mikoa ya Ruvuma, Njombe, Lindi na Mtwara uliofanyika leo Aprili 13, 2026 katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Waziri Dkt. Homera ameongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia na kutoa mafunzo mara Kwa mara kwa wajumbe wa Bodi za Wadhamini ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba na sheria.

Kwa upande wake, Kabidhi Wasii Mkuu Bw. Frank Kanyusi amesema serikali imeamua kutoa mafunzo baada ya kubaini changamoto katika utekelezaji wa majukumu ya wajumbe wa Bodi za Wadhamini kutokana na baadhi yao kutokufahamu sheria, taratibu na mipaka yao katika utendaji wa majukumu yao.

Pia, amebainisha kuwa, baadhi ya Wajumbe wa Bodi za Wadhamini katika taasisi mbalimbali wamekuwa wakijimilikisha mali, kufuja mali na kukaa katika madaraka hayo kwa muda mrefu na kusababisha migogoro isiyokwisha.

RITA inaendelea kutoa mafunzo na elimu kwa Wajumbe wa Bodi za Wadhamini katika mikoa yote ya Tanzania bara ambapo mpaka sasa mikoa iliyopatiwa mafunzo hayo ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa, Manyara, Katavi, Kigoma, Tabora, Rukwa, Songwe na Mbeya