Naibu kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie amesema kuwa kila mtumishi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) anatakiwa kufahamu huduma zote ili kuwa na wigo mpana wa kutoa elimu na huduma kwa wananchi wa makundi yote katika kila Wilaya Tanzania Bara.
Bi. Lesulie amesema hayo leo Septemba 02, 2025 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo maafisa Usajili kuhusu huduma za Ufilisi na Udhamini.
Pia, Bi. Lesulie amewakumbusha wajibu wao watumishi wote huku akisisitiza takwa la kisheia linalompa mamlaka Kabidhi Wasii Mkuu kama mdhamini mkuu wa umma mwenye mamlaka ya kusimamia Mali zisizokuwa na mwenyewe katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara.
"Hii ni huduma nyeti hivyo tuwe makini na wazalendo kusimamia jukumu hilo na kuhakikisha tunatoa elimu na kuzitambua mali zote ili tuweze kuchukua hatua kulinda haki na kuhakikisha mali hizo haziangukii kwenye mikono isiyokuwa salama ya watu wenye nia ovu".Alisema Bi. Lesulie.
RITA imeandaa na kuratibu mafunzo hayo kwa lengo la kuwaongezea ujuzi ili kuboresha huduma za ufilisi na udhamini katika ofisi zote ngazi ya