|
||||||
Date: Author: Jafari Malema
MKUTANO WA TATHIMINI YA MKAKATI WA USAJILI WA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KWA MKOA WA MWANZA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi Emmy Hudson akitoa hotuba kuhusu mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Mkakati wa Usajili wa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano (5BRI) uliozinduliwa mwezi Juni 2015 Mkoa Mwanza, Mkutano wa tathimini ya Mkakati huo unaoendelea katika Hoteli ya Golden Crest Jijini Mwanza.
Mkutano huo umehudhuriwa na Wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii, UNICEF, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa wilaya pamoja na Watumishi kutoka RITA.
|