Swahili   |   English
Usajili wa Vifo

Kifo hutakiwa kusajiliwa ndani ya siku 30, hata hivyo sheria inaruhusu usajili uliochelewa. Jukumu la kusajili wa vifo liko katika wafuatao:

 • Daktari aliyethibitisha kifo, au
 • Ndugu wa karibu wa marehemu ambao walikuwepo wakati wa kifo chake au walikuwepo wakati wa mwisho wa ugonjwa wake, au
 • Mmiliki wa nyumba, au mkazi wa nyumba, au mtu yeyote aliyechukua jukumu la kumzika marehemu huyo.

1: Usajili wa kifo ndani ya siku 30

  Iwapo kifo kimetokea hospitalini, kwenye kituo cha afya au katika zahanati, hakikisha unapata Kibali cha Mazishi. Ikitokea kifo kimetokea nyumbani toa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji, au kwa Msajili wa Wilaya kupata kibali cha mazishi. Jambo hili lifanyike ndani ya siku 30.


2: Taratibu za kupata cheti cha kifo

 • Wasilisha kibali cha mazishi kwa Msajili wa wilaya ambaye kifo kimetokea katika eneo lake la utendaji.
 • Lipa ada inayotakiwa kupata cheti (ada ya sasa ni Tsh. 3500/=).


3: Usajili wa kifo uliochelewa

 • Jaza na wasilisha Fomu D3, ambatisha nyaraka za kuthibitisha (kumbukumbu za kikao cha familia na Barua kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazohusika mfano Kata, Ofisa Mtendaji, Ofisa Mtendaji wa Kijiji) kuthibitisha kifo hicho.
 • Wasilisha picha ndogo ya mwombaji
 • Lipa ada inayotakiwa (ada ya sasa ni Tsh. 4000/=) iwapo kifo kina zaidi ya siku 30 na chini ya miaka 10.  Iwapo kifo kina zaidi ya miaka 10 ada ni Tsh. 10,000/=).


4: Uthibitisho wa kuzaliwa/Vyeti vya vifo

 • Wasilisha nakala ya cheti husika.
 • Lipa ada inayotakiwa (ada ya sasa ni Tsh. 3000/=).

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti

 • Wasilisha maombi ya masahihisho.
 • Ambatisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako.
 • Wasilisha cheti kinachotakiwa kufanyiwa masahihisho.
 • Lipa ada inayotakiwa pale maombi yanapokubalika (ada ya sasa ni Tsh. 6500/= ambapo 3000/= ni ada ya masahihisho, 1,500/= ada ya utafutaji na 2000/= ada ya cheti).

>>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIFO