Miunganisho ya Wadhamini unaviwezesha vyombo visivyoshirikishwa kuwa na uwezo binafsi wa kisheria wa kufungulia na kufunguliwa shitaka katika jina la asasi, kumiliki mali na kuachia mali.
Wasilisha picha ndogo 3 za wadhamini waliopendekezwa, na wasifa wao.
Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo chombo hicho kina makao yake makuu.
Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika sekta ya Serikali ambapo asasi inayotaka kuunganisha wadhamini wake inaangukia (kama ni asasi isiyo ya kidini).
Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika asasi kuu za kidini iwapo kinachoomba ni asasi ya kidini.
Lipa ada halisi/ada ya sasa ni Tsh. 200,000/=.
Tanbihi:
1: Msimamizi Mkuu wa Wadhamini halazimika kuunganisha muunganisho wa Wadhamini pindi mahitaji ya hapo juu yasipotekelezwa.
Nyaraka zote zinazowasilishwa ziwe Nakala mbilimbili isipokuwa Barua ya Mapendekezo.
Mara baada ya kuunganishwa, muunganisho huu unakuwa na wajibu ufuatao:
Hairuhusiwi kumiliki ardhi au haki kwenye ardhi, bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa wadhamini (Kabidhi Wasii Mkuu).
Kumtaarifu Msimamizi Mkuu wa wadhamini juu ya mabadiliko yoyote, mabadiliko ya wadhamini, jina la chombo, anwani ya posta, Katiba ndani ya mwezi mmoja.
Kuwasilisha marejesho ya wadhamini kujaza fomu T.1.5 kila baada ya muda wa miezi kumi na miwili .
2: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo/au marekebisho yoyote kwa ujumla. Taratibu / Mahitaji