USAJILI WA NDOA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ina jukumu la kusajili ndoa kwa kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za ndoa nchini Tanzania na kusajili talaka kwa kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za talaka zinazopokelewa kutoka mahakamani.
Usajili wa Ndoa na Talaka unaongozwa na Sheria ya Ndoa Sura ya 29 Toleo la 2019. Ili kupata huduma yetu mtandaoni mwombaji anatakiwa kujisajili kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na bofya menyu ya eRITA kuchagua neno lililoandikwa Sajili hapa katika huduma za ndoa na talaka ili kujisajili kwenye mfumo.
Jinsi ya kufanya maombi ya huduma mbalimbali:-
1. MAOMBI YA SHAHADA YA KUTOKUWEPO PINGAMIZI
Ni nyaraka inayotolewa na Msajili Mkuu wa ndoa kuthibitisha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hana rekodi ya ndoa na hivyo ana sifa za kuolewa nje ya nchi.
Mahitaji yanayohitajika ili kupata shahada ya Kutokuwepo pingamizi:
-Cheti cha kuzaliwa na pasipoti ya mwombaji,
-Barua ya uthibitisho kutoka kwa mzazi/mlezi,
-Kitambulisho cha mzazi/mlezi
-Pasipoti/kitambulisho cha mtarajiwa anayekusudiwa
Jinsi Maombi yanavyofanyika
- Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka kujisajili na kujaza fomu ya maombi ya mtandaoni (RGM12), maombi yakishatumwa mtandaoni, mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo. Gharama ni Tsh 300,000/=
- Waombaji watajulishwa kupitia akaunti yao ikiwa maombi yao yamekubaliwa au kukataliwa, Wanaweza pia kufuatilia hali ya maombi yao kupitia mfumo wa mtandaoni.
2. MAOMBI YA LESENI YA KUFUNGISHA NDOA.
Leseni ya kufungisha ndoa ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu wa Ndoa ikimpa kiongozi wa dini mamlaka ya kufungisha ndoa. Msajili Mkuu anaweza kufuta leseni ya kufungisha ndoa wakati wowote kwa chapisho la kwenye Gazeti la Serikali
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka kujisajili atajaza fomu ya maombi ya mtandaoni (RGMF 2) na kuambatisha nyaraka zilizoanishwa mtandaoni
- Sharti la awali la kusajiliwa ni kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Dini kusajiliwa katika mfumo wa RITA.
- Mfumo utatoa namba ya malipo kwa Mwombaji na Mwombaji atalipa ada ya maombi. Malipo ni Tsh 60,000/=
3. KIBALI MAALUM CHA MSAJILI MKUU
Msajili Mkuu anaweza kutohitaji taarifa ya kutangaza nia ya kufunga ndoa kama matakwa ya Sheria ya Ndoa inavyotaka pale ambapo kuna sababu ya kutosha ya kutotangaza nia kwa kufanya maombi kwa kuambatisha nyaraka zinazohitajika.
Jinsi ya kufanya maombi:-
- Mwombaji Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kuingia kwenye tovuti www.rita.go.tz na kubonyeza kitufe cha eRITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka na kujisajili atafanya maombi mtandaoni na kuweka ushahidi wa nyaraka juu ya sababu za kwa nini anakwepa kutangaza nia ya siku 21 ya kuoa.
- Maombi yanaweza kukubaliwa au kukataliwa
- Malipo yatafanywa baada ya maombi kukubaliwa na kulipiwa pesa ya Tsh 200,000/=
- Kibali kitatolewa
4. MAOMBI YA KIBALI CHA KUFUNGA NDOA MAHALI MAALUM
Msajili Mkuu anaweza kutoa kibali cha kufunga ndoa mahali maalum tofauti na mahali palipozoeleka kutumika kama mahali pa ibada au mikusanyiko baada ya kupokea maombi ya wenzi wanaotegemea kuoana.
Jinsi ya kufanya maombi:-
- Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuendelea kujaza fomu na kuambatisha nyaraka. Mwombaji lazima aeleze mahali alipokusudia kufungia ndoa yake na kutuma fomu ya maombi mtandaoni na nyaraka za kuthibitisha maombi.
- Mwombaji atalipia Tsh 200,000/=
Kibali kitatolewa.
5. MAOMBI YA KIBALI CHA KUTOKUWA NA NDOA
Ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu kuthibitisha kuwa muombaji wa hati hiyo kuwa hana ndoa.
Mahitaji yanayohitajika ili kupata kibali cha kutokuwa na ndoa:
-Cheti cha kuzaliwa na pasipoti ya mwombaji,
-Barua ya uthibitishaji kutoka kwa mzazi/mlezi,
-Kitambulisho cha mzazi/mlezi
Jinsi ya kufanya Maombi: -
- Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuambatisha nyaraka zake, mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo.
- Mwombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa, Anaweza pia kufuatilia hali ya maombi kupitia mfumo wa mtandaoni.
- Kibali kitatolewa baada ya kulipia Tsh 200,000/=
6. USAJILI WA NDOA ZILIZOFUNGWA NJE YA NCHI
Msajili Mkuu ana mamlaka ya kusajili ndoa zilizofungwa nje ya nchi.
Jinsi ya kufanya Maombi: -
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zilizoanishwa kwenye mfumo
- Cheti kitakachoambatishwa kama hakikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili kinapaswa kiambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa nchi kinapotoka au na BAKITA kwa Tanzania.
- Mwombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 200,000/=
- Cheti kitatolewa.
7. NIA YA NDOA (INTENTION TO MARRY)
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 sura 29 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 inaelekeza kwa mwanamke na mwanaume wanaotarajia kufunga ndoa ni wajibu wa kutangaza nia ya kufunga ndoa siku 21 kabla siku ya kufunga ndoa.
Mahitaji ya nia ya ndoa
- Picha aina ya passpoti ya wanandoa watarajiwa
- Vitambulisho au hati za kusafiria za wanandoa watarajiwa
- Kibali cha kutokuwa na ndoa (kuonyesha hali ya ndoa) kwa raia wa Kigeni
- Barua ya utambulisho toka ofisi za mtaa
Jinsi ya kufanya Maombi: -
- Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuambatisha nyaraka zake
- Mwombaji lazima aeleze mahali alipokusudia kufungia ndoa yake na kutuma fomu ya maombi mtandaoni na nyaraka za kuthibitisha maombi.
- Mwombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa, Anaweza pia kufuatilia hali ya maombi kwenye mfumo.
- Mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo y ash. 100,000 kwa ajili ya kulipia gharama za kufunga ndoa ofisi ya mkuu wa wilaya.
8. USAJILI WA TALAKA
Msajili Mkuu anatoa cheti cha talaka kwa maombi ya wahusika baada ya mahakama kutoa talaka. Huduma ya talaka hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa kwa kutoa cheti cha talaka.
Mahitaji yanayohitajika ili kufanya maombi ya cheti cha talaka
- Hukumu
- Hati ya Talaka
- Cheti cha ndoa
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo
- Sharti la awali ni hukumu ya talaka lazima iwe imetolewa na mahakama yenye uwezo na mamlaka na kuwe hakuna rufaa au muda uliowekwa wa rufaa utakuwa umeisha
- Muombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa,
- Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 40,000/=
- Cheti cha Talaka kitatolewa.
9. TALAKA ILIYOTOLEWA YA NCHI
Maamuzi ya mashauri ya ndoa yaliyotolewa na mahakama zenye mamlaka za nchi za nje yatatambulika na kusajili nchini. Tanzania.
Mahitaji yanayohitajika ili kufanya maombi
- Hukumu ya kuvunja ndoa/ kubatilisha
- Hati ya talaka ambapo haki ya kukata rufaa haipo tena na iwapo haikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au kiswahili inapaswa iambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa mamlaka husika.
- cheti cha ndoa
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo
- Mwombaji katika maombi yake lazima aainishe ni mahakama ya nchi gani iliyotoa hiyo talaka.
- Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh. 200,000/=
- Cheti cha Talaka kitatolewa.
>>> ADA YA HUDUMA ZOTE ZA USAJILI WA NDOA NA TALAKA
NA
|
AINA YA HUDUMA
|
ADA (Tzs)
|
1
|
Cheti cha Ndoa cha Msajili Mkuu wa Ndoa
|
40,000/=
|
2
|
Cheti cha Ndoa ambayo haijawahi kuandikishwa (Subsisting Marriage)
|
40,000/=
|
3
|
Cheti cha ndoa iliyofungwa nje ya nchi (Foreign Marriage)
|
200,000/=
|
4
|
Cheti cha Talaka
|
40,000/=
|
5
|
Cheti cha Talaka iliyotolewa nje ya nchi
|
200,000/=
|
6
|
Leseni ya kufunga ndoa mahali maalum
|
200,000/=
|
7
|
Shahada ya kutokuwepo pingamizi (Certificate of No Impediment)
|
300,000/=
|
8
|
Barua ya kutokuoa/kutokuolewa
|
200,000/=
|
9
|
Uthibitisho wa Cheti cha Ndoa au Talaka
|
40,000/=
|
10
|
Ada ya upekuzi katika daftari la Ndoa/Talaka
|
50,000/=
|
11
|
Kuandikisha uthibitisho wa ndoa iliyobadilishwa kuwa ya mke mmoja au ya wake wengi
|
40,000/=
|
12
|
Marekebisho katika cheti cha ndoa na talaka
Ada ya Upekuzi
Ada ya Marekebisho
Ada ya Cheti cha Msajili wa ndoa na talaka
|
40,000/=
50,000/=
|
13
|
Leseni ya Kufungisha Ndoa
|
60,000/=
|
14
|
Ndoa ya haraka
|
200,000/=
|
15
|
Ada ya ruhusa ya kufungisha Ndoa mahali maalum kwa mgonjwa
|
20,000/=
|
16
|
Ndoa ya Serikali ya kutangaza siku 21
|
100,000/=
|
17
|
Shahada ya ndoa zinazotolewa kwa
wasajili wa wilaya na viongozi wa
dini:-
Shahada 10
|
200,000/=
|