Swahili   |   English
SALAMU ZA PONGEZI
Date: 05 November, 2015 Author: Jafari Malema

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Magufuli ameapishwa na kuanza kazi rasmi hii leo Jijini Dar es salaam.

Rais  wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe  Dk John Pombe Magufuli aapishwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam

Rais Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameapishwa hii leo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande kwenye uwanja wa Uhuru  jijini Dar es salaa na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka huu.

  Marais na wawakilishi wa nchi mbalimbali  walihudhuria katika sherehe za kuapishwa kwake  akiwemo Rais Robert Mugabe wa Zamibabwe, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Joseph Kabila wa DRC Congo, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyata wa Kenya, Philipe Nyusi wa Msumbiji,  Edgar Lungu wa Zambia na Mabalozi wa  mataifa ya Ulaya, Marekani na taasisi za kimataifa ambao wameshuhudia sherehe hizo.

Dk.John Pombe Magufuli anakuwa rais wa awamu ya tano baada ya kupokea kijiti kwa watangulizi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na sasa Dk. Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyemuachia kijiti Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan.