Swahili   |   English
Bodi Mpya ya ushauri ya RITA yazinduliwa
Date: 26 November, 2015 Author: Jafari Malema

Katibu Mkuu- Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Maimuna Tarishi akimkabidhi nyaraka kuhusu RITA Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya ushauri ya Wakala Prof. Hamisi Dihenga katika hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa RITA, Jijini Dar

Bodi mpya ya Ushauri ya RITA yazinduliwa

Katibu Mkuu-Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi amezindua bodi mpya ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini ( RITA) katika hafla iliyofanyoka katika Ofisi za Makao Makuu ya Wakala jijini Dar es Salaam. Bodi hii ni ya Tatu tangu kuanzishwa RITA itakayokuwa chini ya Uenyekiti wa Prof. Hamisi Dihenga na inachukua nafasi ya bodi ya pili ambayo imemaliza muda wake kwa mujibu wa Sheria.

Katika uzinduzi huo Bi. Tarishi aliwapongeza wajumbe wote kwa kuweza kuteuliwa na kuwataka kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na miongozo lengo lao kuu likiwa kuiwezesha RITA kuongeza ufanisi katika utoaji huduma bora kwa wananchi. Pia aliongeza kwamba wananchi wana matarajio makubwa kutoka RITA kwani huduma wanazotoa zinamgusa kila mwananchi hivyo Bodi ishirikiane na Manejimenti ya Wakala kuhakikisha matarajio yanatimizwa.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi iliyomaliza muda wake menejimenti ya RITA na Wajumbe wanane wa  Bodi mpya  ambayo itakuwa kazini kwa muda wa Miaka 4.