Swahili   |   English
UZINDUZI WA KAMPENI YA KUTOA ELIMU NA USHAURI WA KISHERIA BURE KUHUSU MASUALA YA WOSIA NA MIRATHI MKOANI ARUSHA.
Date: 03 June, 2016 Author: Jafari H.Malema

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Fadhili Nkurlu akiwahutubia Wananchi wakati wa ufunguzi wa kampeni ya utoaji elimu na huduma ya kuandika na kutunza Wosia iliyofunguliwa wiki hii Jijini Arusha, kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Daniel Machunda

Wakala wa usajili ufilisi na udhamini (RITA) umewataka wananchi kuandika wosia kipindi hiki wakiwa na afya njema ili kuepusha watoto, mjane au mgane na ndugu kuingia katika  migogoro ikitokea  mmojawapo  kutangulia mbele za haki.