Swahili   |   English
MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA KUANZISHWA KWA RITA
Date: 24 June, 2016 Author: Jafari H.Malema

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson (wa tatu kutoka Kushoto) akimbemba mmoja wa Watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam siku ya Maadhimisho ya Miaka Kumi ya kuanzishwa Wakala wa RITA. Watoto hao walisajiliwa na k

RITA YAAADHIMISHA MIAKA KUMI (10) YA KUANZISHWA WAKALA NA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeadhimisha Miaka 10 tangu kuanzishwa pamoja na Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma hapo jana tarehe 23 Juni 2016.

Kwa pamoja  maadhimisho hayo yaliambatana na matukio yafuatayo:

1)      Kusajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wote waliozaliwa siku ya Tarehe 23 Juni 2016 katika Hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam. Pia Elimu kuhusu Huduma za Wakala kwa wananchi katika eneo hilo.

 

2)      Kuanzisha Dawati maalumu katika Ofisi ya Makao Makuu ya RITA kwa ajili ya kupokea Malalamiko, maoni, kero za Wananchi. Pia Dawati hilo limetoa Elimu kwa wananchi kuhusu huduma za Wakala.

 

3)      Kutoa Elimu kwa Umma kwa Wananchi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani.

 

RITA inawashukuru Wadau wote walioshirikiana na Wakala katika kipindi cha Miaka Kumi (10) iliyopita.