Description:
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Bw Amon Mpanju akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau kutoka Nchini Ghana, Marekani na mashirika ya Kimataifa ya maendeleo waliokutana hii leo Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujadili Mifumo mbalimbali ya kisheria inayosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na Ukusanyaji wa takwimu,kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtenjaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson na kushoto kwake ni Msajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu kutoka Marekani state ya Hawii Bw Alvin Onaka Mwingine ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Erica Yegela.