Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           MAKUBALIANO- UHAMIAJI NA RITA

Description: Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Idara ya Uhamiaji zimesaini hati ya makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ya utambuzi wa nyaraka kwa njia za kisasa za kidijitali ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi wanaoomba vyeti vya kuzaliwa na pasi za kusafiria. Akipongeza hatua hiyo hii leo Jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Wahamaji, Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Mhandisi. Hamad Masauni amesema kuwa hatua hiyo itarahisisha utoaji wa huduma kwa haraka kutokana na matumizi ya TEHAMA katika kuhakiki taarifa za wananchi wanaoomba pasi za kusafiria.

Album Pictures