Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           RITA YAKABIDHI MALI MBEYA CLUB

Description: Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu (RITA) imekabidhi rasmi Mali za Mbeya Club kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuzisimamia na kuziendesha. Makabidhiano yamefanyika Mkoani Mbeya kwa kusaini Mkataba wa Makabidhiano wa mali kati ya Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ikiwakilishwa na Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Emmy Hudson na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya iliyowakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Dr. Salum Manyata. RITA ilikabidhiwa mali za Mbeya Club kama Mdhamini wa Umma baada ya kufungua shauri Mahakama Kuu kuomba kuzisimamia mali za iliyokuwa Mbeya Club kutokana na Bodi yake ya Wadhamini kutowasilisha marejesho ya kila mwaka na hivyo kutokuwa hai kwa zaidi ya miaka 35 na hivyo kukosa uhalali wa kisheria wa kuendelea kusimamia mali za Taasisi hiyo. Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya iliridhia ombi hilo kupitia Hukumu iliyotolewa na Mheshimiwa Jaji Dustan Ndunguru ya tarehe 26 Juni 2019 na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kupewa usimamizi wa mali za taasisi hiyo kama Mdhamini wa Umma (Public Trustee).

Album Pictures