Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           KAMPENI WILAYA YA ARUSHA MJINI

Description: KAMPENI YA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WAKAZI WA WILAYA YA ARUSHA YAZINDULIWA. Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi Amezindua kampeni ya siku kumi ya kusajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa wa wakazi wa wilaya yake ambayo imeandaliwa na ofisi yake, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini ( RITA) na Mbunge wa Jimbo la Arusha. Amewataka wananchi kutumia fursa hii iliyotolewa kuhakikisha wanapata vyeti vya kuzaliwa kwani huduma hii imewafata katika maeneo yao wanayoishi. Lengo la kampeni hii ni kupunguza changamoto ya wananchi wengi kukosa vyeti vya kuzaliwa ambayo ni nyaraka muhimuhimu kwa mwananchi kwa ajili ya kupata huduma nyingine. Kampeni inafanyika katika vituo vitatu ambavyo ni : -Stendi ya Hiace Kilombero -Shule ya Msingi Moshono -Ofisi ya Mtendaji Kata Muriet

Album Pictures