Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           Kamati ya Katiba na Sheria

Description: Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imetoa wito kwa wananchi kuandika na kuhifadhi wosia katika Taasisi ya RITA ili kuepuka migogoro ndani ya familia inayosababishwa na ndugu kulazimisha kurithi mali za marehemu kinyume na taratibu na Sheria zinazosimamia masuala ya mirathi. Akizungumza hii leo katika kikao cha kamati Jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewahimiza Wabunge wote ambao bado hawajaandika Wosia kufanya hivyo ikiwa kama sehemu ya kuwahamasisha wananchi wao kuchukua hatua mapema na kulifanya jambo hilo kuwa ni kipaumbele hasa ukizingatia migogoro na kesi nyingi zinazohusu mirathi zinatokea katika majimbo yao. "kwa kiasi kibubwa migogoro mingi hutokea na ukifuatilia chanzo chake unabaini kinasababishwa na kutoachwa muongozo unaotoa maelekezo kuhusu mgawanyo wa mali za marehemu".Alisema Mhe. Mchengerwa.

Album Pictures