Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           Usajili wa vifo Mkoa wa Mbeya

Description: Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuacha mara moja utaratibu wa kuzika wapendwa wao pindi wanapofariki bila kuzijulisha mamlaka zinazohusika katika eneo wanakoishi na kusababisha Serikali kuchelewa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na sababu za vifo hivyo pamoja na upatikanaji wa takwimu sahihi za matukio hayo. Agizo hilo limetolewa hii leo Jijini Mbeya na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Albert Chalamila kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya zake iliyoandaliwa na kuratibiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuhusu kutambulisha rasmi Mfumo ulioboreshwa wa Usajili wa Vifo

Album Pictures