Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Picha za Albamu
Album:           KIKAO CHA TATHMINI

Description: *RITA YAHAKIKI VYETI 111,358 VYA WANAFUNZI WANAOOMBA MIKOPO YA ELIMU YA JUU. -Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umefanikiwa kuhakiki jumla ya vyeti 111,358 vya Kuzaliwa na Vifo ambapo jumla ya maombi ya Kizazi 96,329 sawa na asilimia 95 yalihakikiwa na jumla ya maombi ya Kifo 15,029 sawa na asilimia 94 yalihakikiwa kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2021/22. Hayo yametamkwa na mwakilishi wa Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu, ambaye ni Afisa Usajili, Beatrice Mboya katika kikao cha tathmini kilichoandaliwa na Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo hii jijini Dar Es Salaam. -Katika taarifa yake, Bi.Mboya amesema kuwa kutokana na maboresho yaliyofanyika katika ukurasa wa Wakala Huduma mtandaoni, imewarahisishia wanafunzi wengi kuweza kukamilisha suala zima la uhakiki huo bila kujali umbali wa mahali walipo kwani kilakitu kinafanyika mtandaoni. -Akiongelea changamoto wanazozipata, Bi,Mboya amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa hawazingatii maelekezo husika kutoka RITA pale wanapotuma maombi yao kwani wengine badala ya kutuma cheti kinachotakiwa kuhakikiwa wanatuma picha au CV na wakati huohuo wengine wanapotuma cheti hawakiweki katika mfumo wa PDF hivyo inakuwa ngumu kufanyiwa kazi kwa wakati. -"Zoezi la uhakiki bado linaendelea na hivyo basi tunapenda kusisitiza wanafunzi wetu kuzingatia vigezo vya kukamilisha uhakiki huo pale wanapotuma maombi yao katika ukurasa wa RITA huduma mtandaoni na pale wanapohisi kukwama basi wasisite kuwasiliana nasi kwa simu ya huduma kwa wateja ambayo ni 08001174 au katika kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii ambayo ni facebook,instagram na twitter kwa msaada zaidi" alisema. -Kikao hicho cha tathmini kilihudhuriwa na wadau wa Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambao ni Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Shirika la Posta Tanzania ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa HESLB, Abdul-Razaq Badru.

Album Pictures