Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Picha za Albamu
Album:           HUDUMA PAMOJA

Description: UZINDUZI WA VITUO VYA HUDUMA PAMOJA. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezindua rasmi vituo vya Huduma Pamoja vitakavyojumuisha Taasisi mbalimbali za Serikali katika kutoa huduma zake ndani ya ofisi za Shirika la Posta nchi nzima. Akizungumzia huduma hiyo Mh. Majaliwa amesema kuwa, "Huduma Pamoja" ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Serikali ambapo lengo kuu ni kuweka mazingira rahisi na wezeshi kwa wananchi kuweza kupata huduma zote za Serikali ndani ya eneo moja na kwa muda mfupi. Mhe. Majaliwa amezitaka Taasisi zinazotoa huduma za Serikali kwa wananchi kuongeza kasi ya kujiunga na kutumia "Huduma Pamoja" iliyopo ndani ya Shirika la Posta Tanzania. Baadhi ya Taasisi za Serikali ambazo zinatoa huduma zake ndani ya ofisi za Shirika la Posta ni RITA, NIDA, PSSF, NSSF, NHIF, TRA, Uhamiaji, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CRDB pamoja na BRELLA.

Album Pictures