Swahili   |   English
Image caption.
Image subcaption.
Picha za Albamu
Album:           USAJILI WATOTO MKOA WA RUKWA

Description: Wadau wa masuala ya usajili na utambuzi wa watu wamekutana na kukubaliana kwa pamoja kuhusu vigezo na taratibu za kisheria zilizopo zitakazotumika kuwatambua watoto pamoja na wazazi wao wakati wa utekelezaji wa mpango wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wote wa umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Rukwa. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hii leo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akimuakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo amesema Mikoa yote ya mipakani changamoto zake zinafanana kutokana na miingiliano ya ujirani na kifamilia hali inayopelekea baadhi ya wanafamilia na viongozi wa vijiji na kata kushindwa kutoa ushirikiano wa kupata taarifa sahihi za kuwatambua wananchi waliozaliwa ndani ya mipaka ya Tanzania na wale waliotoka nchi jirani.

Album Pictures