Description:
RITA- NHIF wajadili kuhusu uhakiki wa taarifa zitokanazo na usajili wa matukio ya vizazi, vifo, ndoa na talaka pamoja na watoto wa kuasili ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.
Viongozi hao wamekutana leo tarehe 15/06/2022 katika ofisi za RITA Makao Makuu ambapo Kwa upande wa NHIF umeudhuriwa na Meneja Uanachama, Bi. Salome Manyama, Meneja Masoko na Huduma kwa wateja, Bw. Hipoliti Lello na Meneja Huduma za Tehama, Bw. Bakari Mhamali. Kwa upande wa RITA Meneja Usajili, Bi. Patricia Mpuya akimwakilisha Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa mtendaji mkuu, Bi. Angela K. Anatory, wengine ni kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Bw. Nicholaus Muhanyiwe, Afisa tehama Bi.Robi Otaigo na Msajili mwandamizi wa ndoa na talaka Bi. Jane Balongo.