Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           MKUTANO MKUU WA MAWAKILI

Description: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro amewataka mawakili wa serikali ya Tanzania kutekeleza majukumu ya serikali kwa kuzingatia sheria kwa maendeleo ya nchi. Dkt. Ndumbaro ameongea hayo leo tarehe 30 Septemba 2022 wakati akifunga mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma. Ameongeza na kusema kuwa "katika kauli mbiu yenu nimeona kuna mambo kadhaa ikiwemo uzingatiwaji wa sheria hivyo sisi kama mawakili wa serikali tuhakikishe tunazingatia sheria na haki kwa maendeleo ya Taifa letu la Tanzania na kusaidia kuepukana na migogoro mbalimbali inayosababishwa na ukosefu wa haki katika jamii yetu". Mawakili kutoka RITA wameshiriki kikao hicho kilichofanyika kwa siku tatu huku Wakala ukitoa huduma ya Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa, msaada wa kisheria kuhusu kuandika na kuhifadhi Wosia na Mirathi pamoja na elimu kwa umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na RITA. Aidha, Dkt. Ndumbaro amewataka mawakili hao wa serikali kutunza siri za serikali na kujikita zaidi katika matumizi ya TEHAMA yanayozingatia sheria na weledi na kuepuka kutumia vibaya mitandao kuchafua sifa ya serikali.

Album Pictures