Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           WIKI YA SHERIA 2023

Description: RITA YASHIRIKI WIKI YA SHERIA 2023. Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA)unashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika kuanzia tarehe 22 -31 Januari 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani Dodoma, Viwanja vya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam pamoja na viwanja vya General Mayunga mkoani Kagera. Wiki ya Sheria imezinduliwa leo ambapo Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kitaifa mkoani Dodoma alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango. Katika mabanda ya RITA huduma mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu huduma za Wakala, ushauri wa kisheria bure kuhusu Wosia na mirathi, Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa pamoja na maelezo ya kina kwa Bodi za wadhamini wa Taasisi kuhusu namna ya kuhuisha katiba zao.

Album Pictures