Swahili   |   English
Picha za Albamu
Album:           RITA AWAY DAY 2024

Description: Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi Juni 23, 2024 ametoa maagizo kwa watumishi wote wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma pamoja na kuchapa kazi kwa kuzingatia weledi, ubunifu na kutanguliza uzalendo katika kutoa huduma bora kwa Wananchi. Bw. Kanyusi ameyasema hayo Jijin Dar es Salaam wakati akizungumza na Wafanyakazi katika mkutano wa mwaka uliojumuisha watumishi kutoka Wilaya zote hapa nchini. "Fanyeni kazi kwa bidii na kujituma huku mkitambua sheria na kanuni za utumishi wa umma, jiepusheni na vitendo vya rushwa, kauli mbaya kwa wateja na utoro kazini kwani hivyo vyote husababisha kuwakosesha haki wananchi lakini pia ni utovu wa nidhamu kwa mtumishi wa umma." Alisema Bw. Kanyusi. Kwa upande wake Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie amesema kwa sasa mazingira ya utoaji huduma yanaendelea kuboreshwa kwa wafanyakazi na hivyo kuhakikisha muda na rasilimali zilizopo zinatumika vizuri katika kutekeleza majukumu ya kila siku. " Wote ni mashahidi tumepatiwa watumishi wapya na kwa upande wetu tumewapatia vitendea kazi zikiwemo kompyuta mpakato ili kuwezesha kutoa huduma kidijitali kupitia eRITA katika Wilaya zote." Alisema Bi. Lesulie.

Album Pictures