Description:
Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi leo Agosti 03, 2024 amekagua Banda la RITA kwenye maonesho ya wakulima Nanenane Jiji Dodoma na kuridhishwa na shughuli za utoaji huduma na elimu kwa umma.
Pia, Bw. Kanyusi ameongea na wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma ya usajili wa vizazi na vifo na kisha kukabidhi vyeti vya kuzaliwa kwa baadhi ya wananchi hao.
Wakati huo huo amewataka wananchi kuwa mabalozi na kuwafikishia taarifa na elimu waliyoipata ndugu, jamaa na majirani zao ili nao wapate haki yao ya msingi ya kusajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa.