RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Naibu Waiziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakiwa na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai wamefanya ziara katika kituo cha afya Makuburi jijini Dar es salaam na kukagua maendeleo ya Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya Miaka mitano.
Mpango huo ni sehemu ya ufadhili wa serikali ya Canada kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF ambapo watoto wa umri huo wanasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bila ya malio katika vituo vya tiba ya afya ya uzazi na mtoto pamoja na ofisi za watendaji kata na tayari utekelezaji wake unaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara.