Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Dkt Rehema Nchimbi ameagiza Wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani humo kusajiliwa na kupatiwa vyeti  vya kuzaliwa kabla ya kuhitimu.
Maagizo hayo yametolewa leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo  ya siku moja kwa Waratibu Elimu Kata kuhusu mpango wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa  wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Singida Mkoani humo.