Wizara ya Katiba na Sheria Imeridhishwa na utendaji kazi wa  Bodi ya Ushauri ya Wizara hiyo inayomaliza muda wake  kwa kufanikiwa kusimamia na kutekeleza maagizo yote manne  yanayohusu Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA).
Akizungumza hii leo Jijini Dar es salaam wakati wa kupokea Taarifa ya Bodi inayomaliza Muda wake  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Prof. Palabagamba Kabudi amesema kuwa Bodi hiyo imetekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kusimamia na kuishauri Wizara kuhusu utendeji kazi wa  RITA.