Zaidi ya wanachama wa 200 VICOBA kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam na mikoa jirani hii leo wamepatiwa elimu juu ya usajili na utoaji wa vyeti  vya kuzaliwa, Ndoa na Talaka kwa lengo la kuwasaidia wakati wa shuguli zao za ujasilia mali ikiwemo  mikopo, kumiliki mali , ardhi pamoja na haki ya kurithi mali  ya mwenza pindi inapotokea  amefariki dunia.